logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Siwezi kumuacha Laureen!" Jamaa wa miaka 25 ataka kusaidiwa kumshawishi mama mtoto awe mke wa pili

"Ata mtoto si wako, akishazaliwa ni wa kila mtu. Mimi ndiye naweza kuamua ataenda kwa familia gani," Beatrice alimwambia Michael.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho05 November 2024 - 08:37

Muhtasari


  • Michael alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Novemba mwaka jana kufuatia masuala kadhaa katika mahusiano yao.
  • "Nilikwambia huyo msichana siwezi kumuacha, na pia wewe uko katika maisha yangu. Hii ni kitu ambacho nimeamua kufanya," Beatrice alimwambia Michael.



Michael Oduor, 25, kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Beatrice Odhiambo ,27, ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka uliopita.

Michael alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Novemba mwaka jana kufuatia masuala kadhaa katika mahusiano yao.

Pia alikiri kwamba ana uhusiano na mwanadada mwingine ambaye hataki kumwachilia kutoka katika maisha yake.

"Nilikutana na Beatrice miaka tatu iliyopita. Mi ni msanii, ila niliwacha kwa sababu yake. Tulikutana, tukapendana, kidogo kidogo akapata mimba akaja tukae. Akaanza tabia za wanawake baada ya kupata mimba. Alikuwa na mabadiliko ya hisia. Wakati alikuwa na mimba, nilikuwa nafanya kazi kwa hospitali, pesa ilikuwa inachelewa, ikawa ngumu kumtunza kwa nyumba. Tukaongea naye nikamuuliza kama anaweza kuenda nyumbani. Alienda kwa shangazi, akazaa," Michael alisimulia.

"Pia kuna huyu mwanadada, alikuwa mwanamke wangu, nilipenda kuongea sana naye. Huyo mwanadada alipenda kupiga simu sana usiku. Ni mwanamke wangu pia, huyo ndiye alifanya tukakosana na huyo mwanamke wangu mwenye ako na mtoto. Kwa sasa mama mtoto amenuna na mimi, haongei na mimi. Nilishamwambia kuhusu huyo mwanadada. Nataka kuwa na wanawake wawili," aliongeza.

Haya yalimshangaza sana Gidi ambaye alisema, "This is a confused Gen-z!"

Beatrice alipopigiwa simu, Michael alichukua nafasi hiyo kuomba msamaha.

"Naomba sana unisamehe. Siko sawa kabisa, ndio maana nimekuja hapa,'" Michael alisema.

Beatrice ambaye alisikika kuwa na hasira aliweka wazi kwamba hataki mambo ya Michael huku akibainisha kwamba maisha yake yamekuwa sawa bila uwepoo wake.

"Saai sitaki kuongea mbaya. Nilishakwambia sina shida na wewe na huyo msichana,. Na nilikwambia tumekuwa tukisurvive na mtoto bila wewe," Beatrice alisema.

Michael alijibu, "Kama ni suala na fedha, ama Laureen, nilikwambia huyo msichana siwezi kumuacha, na pia wewe uko katika maisha yangu. Hii ni kitu ambacho nimeamua kufanya."

Beatrice alisema, "Ata mtoto si wako, akishazaliwa ni wa kila mtu. Mimi ndiye naweza kuamua ataenda kwa familia gani. Kama unahisi unataka kuwa baba mtoto, angalau ungekuwa unahakikisha unamuona mtoto. Niko na mambo mengi ya kufikiria sio mambo yako tu na huyo msichana. Nimekuwa nikiishi bila wewe. Nyinyi endeleeni kufanya kitu unataka."

"Wacha kuniweka hewani. Nadhani hunijui vizuri. Nimekuwa nikivumilia kwa muda. Nimekuwa nikikupigia simu tuongelee mtoto, wewe unaongelea huyo msichana. Wacha kunifuatilia," aliongeza.

Alituma onyo kali kwa mzazi huyo mwenzake huku akimtaka aache kumsumbua.

"Naelewa huyo msichana alikuwa wake wa kwanza, na sikujua. Mimi nilishamuacha, asiniletee mambo ya huyo msichana," alisema.

Michael alisema, "Sijachanganyikiwa, najua kile ninachofanya.Naomba unielewe, unisikize.":

Laureen alimalizia kwa kusema, "Asante sana, angalau nimejiskia kwa Radio Jambo. Yeye aende akae chini ajiangazie."

Je, una maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved