logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa awaongelesha vibaya mkewe na mama mkwe baada ya kula fare ya Sh20,000

"Huwa ananiambia anakuja, natuma nauli na hakuji. Wakati nilikuwa nawatumia nauli na hakuji, nilikasirika nikawaongelesha vibaya," Ramsey alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho06 November 2024 - 08:37

Muhtasari


  • Ramsey alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika Aprili mwaka huu wakati walipozozana baada ya mke wake kuenda nyumbani na kutorudi.
  • Ramsey aliendelea kufichua kwamba hajawahi kukutana na mama mkwewe licha ya kuwa tayari ana mtoto na bintiye.



Jamaa aliyejitambulisha kama Ramsey Namema ,24, kutoka Mlolongo alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwe wake Jackline Mokaya ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Ramsey alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika Aprili mwaka huu wakati walipozozana baada ya mke wake kuenda nyumbani na kutorudi.

Alisema mkewe alienda nyumbani kwa ajili ya mazishi, ila hakuwahi kurudi licha ya yeye kutuma nauli mara kadhaa.

"Huwa ananiambia anakuja, natuma nauli na hakuji. Wakati nilikuwa nawatumia nauli na hakuji, nilikasirika nikawaongelesha vibaya.. Niliongelesha mama mkwe vibaya," Ramsey alisema.

Aliongeza, "Tuko na mtoto mmoja, tulikuwa tunaishi tu, nilikuwa napanga kuenda kwao mwaka ujao. Tulikuwa tunaongea tu vizuri, nikituma pesa ndo wanaanza madharau. Amekula nauli ya kama 20,000."

Ramsey alisema kwamba wazazi wake tayari wamemuomba kuachana na mkewe ila hataki kwani wana mtoto.

"Nilieleza wazazi, lakini mama mkwe alikataa. Wazazi wananiambia niachana na yeye. Niko na mtoto na yeye, sitaki kumuacha. Hana simu, tunawasiliana kutumia simu ya mama," alisema.

Juhudi za kumpatanisha Ramsey na mama mkwe wake hata hivyo hazikufua dafu kwani simu yake haikuingia alipopigiwa na Gidi.

Ramsey aliendelea kufichua kwamba hajawahi kukutana na mama mkwewe licha ya kuwa tayari ana mtoto na bintiye.

"Tulikutana na yeye akiwa kwa shangazi.Ata sijawahi kukutana na mama yake. Nimempeleka kwetu," alisema.

Katika maneno yake ya mwisho kwa mama mkwewe, Ramsey alisema, "Mama Cynthia, mimi sina ubaya na wewe. Ningependa uambie Cynthia arudi kwake. Sina ubaya. "


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved