logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada amuacha mpenziwe baada ya kukataa kumrejeshea dadake nauli aliyotumia

"Haikuwa lazima niende kwake kwa sababu hakuwa amenioa. Nilimwambia utafute kazi kwanza. Saa hii siko tayari kuolewa," Kariuki alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho12 November 2024 - 08:38

Muhtasari


  • Kariuki alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwaka wa 2022 wakati mkewe aliondoka kwenda nyumbani kwa ajili ya mazishi.
  • "Mimi sitaki hiyo mambo. Mimi siwezi kuskilizwa kwa redio. Sitaki. Kwa nini anipeleke huko jameni?" Ann alisema.

Jamaa aliyejitambulisha kama Samuel Kariuki ,29, kutoka Kirinyaga alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Ann Samanga ,21, kutoka Uganda ambaye alikosana naye takriban miaka miwili iliyopita.

Kariuki alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwaka wa 2022 wakati mkewe aliondoka kwenda nyumbani kwa ajili ya mazishi

"Siku moja aliniambia anaenda mazishi. Akaenda na hakurudi. Tulikuwa tunaishi pamoja Nairobi. Sikuwa nimemkosea. Alibeba nguo zake zote akienda. Aliniambia anaenda siku kadhaa atarudi. Nilifikiria tu anaenda lakini alinishawishi kwamba amewacha zingine," Kariuki alisema.

Aliongeza, "Nimemtumia nauli na hakuji hadi mwishowe akaniweka blacklist. Alikuja na mtoto wake mmoja huyo mwingine alibaki nyumbani. Tuko na mtoto mmoja naye"

Ann alipopigiwa simu, mwanzoni alisita dhidi ya kuzungumza hewani.

Aidha, alibainisha kwamba tayari amekatiza uhusiano wake na Kariuki na akaeleza kwamba walikosa kuelewana kuhusu nauli.

"Mimi sitaki hiyo mambo. Mimi siwezi kuskilizwa kwa redio. Sitaki. Kwa nini anipeleke huko jameni?" Ann alisema.

Aliendelea, "Mimi niliachana naye kitambo. Wakati huo nilikuwa na mimba ikanisumbua. Ilifika mahali nikamwambia anitumie nauli. Nikatumia kununua vitu zingine. Nikamwambia atume tena, hakutuma,  dadangu alinipa nauli lakini alitaka kurudishiwa, nikaenda kwa dadangu.

Hakuwahi kutuma. Hakuwa amenioa rasmi. Ni ile tulijuana. Haikuwa lazima niende kwake kwa sababu hakuwa amenioa. Nilimwambia utafute kazi kwanza. Saa hii siko tayari kuolewa."

Ann hata hivyo alimwambia Kariuki amtafute kwa simu ili waweze kuzungumza.

Kariuki alimalizia kwa kumwambia, "Bado mimi nakupenda. Nitaenda kukupenda. Urudi tuendelee."

Ann alisema hana maneno ya kumwambia Kariuki.

Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved