logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Dereva wa teksi aahidi kumpigia simu mpenziwe kila baada ya masaa 4 ili asimshuku anamcheza

"Nakupenda lakini shida yako unanyamazanga sana. Nakuelewa lakini usinyamazange sana. Mimi sina shida na wewe," Jessyline alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho13 November 2024 - 08:38

Muhtasari


  • Austine alisema ingawa bado hajatengana na mpenziwe huyo wa mwaka mmoja, kumekuwa na shida ya mawasiliano kati yake naye.
  • Austine aliahidi kumtembelea mchumba wake na kurekebisha tabia yake ya mawasiliano mabaya.

Austine Rakhutsi Mangeti ,29, kutoka Mumias alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Jessyline mwenye umri wa miaka 22.

Austine alisema ingawa bado hajatengana na mpenziwe huyo wa mwaka mmoja, kumekuwa na shida ya mawasiliano kati yake naye.

Alisema mpenziwe amekuwa akimshuku kuwa na mpango wa kando tangu alipohamia Nairobi kwa ajili ya kazi ya udereva wa teksi.

"Ni kama ananishuku. Nilikuja kazi Nairobi nikamuacha Kakamega. Anashuku nilikuja Nairobi kutembea na wanawake na mimi nilikuja kazi," Austine alisema.

Aliongeza, "Nataka kumpa hakikisho kwamba mimi sina wanawake wengine na hata nilikuwa nimepanga kwenda kwao Desemba ili kujitambulisha. Mipango bado iko, nataka kwenda kwao tarehe 27 Desemba. Anasema stori za madereva ni mbaya. Sio madereva wote wabaya. Mimi ni dereva wa uber. Mimi huwa najicontrol. Hata nikiwa dereva, sio kila mwanamke atakuwa wangu."

Jessyline alipopigiwa simu, Austine alitumia fursa hiyo kujieleza na kumhakikishia mpenziwe kwamba ye ni mwaminifu.

"Nimeamua leo ikuwe mimi na wewe. Sio eti nakuchezea na wasichana vile unanishuku. Niko kazi," Austine alisema.

Jossyle alijibu, "Nakupenda lakini shida yako unanyamazanga sana. Nakuelewa lakini usinyamazange sana. Mimi sina shida na wewe."

Austine aliahidi kumtembelea mchumba wake na kurekebisha tabia yake ya mawasiliano mabaya.

"Nitarekebisha. Nitakuwa namuongelesha baada ya saa mbili. Nitakuwa nampigia baada ya kila saa nne. Hiyo ni sawa," alisema.

Jossyline alisema, "Nimeridhika lakini aseme na atende. Nakupenda sana. Wewe ni kipenzi cha moyo wangu. Kila kitu umesema utende juu mimi nakupenda sana na moyo wangu wote."

"Nakupenda sana kwa maisha yangu. Naomba Mungu atujalie maisha mazuri ya mbele," Austine alisema.

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved