Brian Omukunga ,27, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwewe Violet ama Mama Kamonye ,45, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.
Brian alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika Januari mwaka huu wakati alipomtumia ujumbe mbaya kwenye simu.
Alisema alimwambia mama mkwewe kwamba alishuku ujauzito wa bintiye sio wake.
"Sikumtukana mama mkwe. Niliandika meseji kuhusu msichana wake wakati alikuwa mjamzito. Niliandika ni kama huyo mtoto sio wangu. Nilikuwa nashuku mtoto sio wangu," Brian alieleza.
Aliongeza, "Msichana alipojifungua, alikuwa ananipigia simu. Mama pia tumekuwa tukiongea lakini sio vizuri Nimeshughulika. Mama ndio tunaongea na yeye, lakini kwa roho kuna vile naona hajanisamehe. Nimeshindwa kumwambia anisamehe."
Brian alisema kwamba mkewe alirejea nyumbani kwao baada ya kuzozana kuhusu mwanaume aliyempigia simu.
"Msichana alirudi kwao. Kulikuwa na shida na mtoto. Wakati alikuja, kuna mwanaume alipiga simu nikachukua. Mwanaume alisema "Hello babe, kwani uko wapi? Mtoto wangu umepeleka wapi?" Ilinishtua sana, sikumpiga ama kumfanyia kitu yoyote. Jamaa alisema tufanye kile tunafanya lakini mtoto tumrudishie," alisema.
:Mtoto ni kijana lakini anafanana na mama. Mtoto siwezi jua kama ni wangu. Kijana aliniambia alipatana na huyo mwanamke mwaka moja umeisha. Alisema msichana alimwambia alikuwa na Brian lakini waliachana," alisema.
Mama Kamonye alipopigiwa simu alibainisha kwamba madai ya Brian ni ya kweli.
Hata hivyo, alieleza kwamba Brian alikataa kushughulikia mtoto na ndiposa bintiye akapata mpenzi mwingine.
"Msichana vile alishika mimba alisema ni ya Brian. Vile alizaa, Brian akakataa kumsaidia, msichana labda akapata mtu mwingine, juu mtu mzuri ni yule anakusaidia," Mama Kamonye alisema.
Brian aliomba msamaha, "Mimi nilikuwa nataka kuomba msamaha kwa ile vitu nilikuandikia. Najua niliandika vitu za makosa ambazo sio nzuri."
Mama Kamonye alimwambia, "Nilishindwa mimi sijakuona na sikujui, na wewe ndiye unanitumia jumbe za ujinga. Nilishindwa unaanza namna gani. Ungetumia yule msichana mlikuwa na yeye. Mimi sikujua."
Alieleza kwamba msichana alirejea nyumbani baada ya kushindwa kustahimili hali kwa Brian.
"Msichana mwenyewe amepanga safari. Nikapata amepotea kwa boma akaenda. Msichana alifika na hata kijana hawezi kusema ako naye. Alikaa huko wiki mbili. Alirudi akaniambia mambo ameona kwa huyo kijana hawezi kurudi. Alisema anataka alee mtoto wake," Mama Kamonye alisema.
Brian alijitetea akisema, "Simu ndiyo ilifanya Kamonye akarudi kwao. Yeye ameenda akasema ati vitu nimefanya ndizo zimefanya aende."
"Kamonye alisema amepata mpenzi ambaye anaweza kumnunulia sabuni na kununulia mtoto pampers. Mimi nilimsamehe kitambo sana. Mimi sijawahi kumrudishia hata siku moja," Mama Kamonye alisema.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?