logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada auma mkono wa mama mkwe baada ya kumzuia kujitoa uhai kutumia dawa

"Wakati nilienda kuchukua vitu zangu, akachukua dawa ameze eti akufe. Mimi nikagonga hiyo dawa kwa mkono yake," Mama Mkwe alieleza.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho21 November 2024 - 09:09

Muhtasari


  • Regina alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika wiki jana  wakati waligombana hadi kupigana kutokana na mzozo wa kinyumbani.
  • "Mbona hajatengeneza nyumba yake kama iko na shida?  Mimi nilitaka aende atengeneze nyumba yake, yeye anauma mimi na meno,” Rose alisema.


Regina Onyango ,37, kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwe wake Rose Otieno Juma ,55, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Regina alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika wiki jana  wakati waligombana hadi kupigana kutokana na mzozo wa kinyumbani.

“Sikupenda kwangu, sikutarajia kumpiga. Kulikuwa na maneno kidogo ya nyumbani

Niliamka asubuhi moja, mama mkwe alikuwa nyuma ya jikoni. Huwa tunapika na yeye mahali pamoja. Hatukuwa tunaongea, ata hatukuwa tumesalimia.

Kuna Jirani nilikuwa nilikuwa nimekosana naye hapo nyuma, nilimsaidia na TV yangu, ikaharibika kwenye mikono yako. Vile niliambia mama mkwe kuhusu TV akaambia Jirani aniletee TV. Tulikuwa tumeelewaana anaenda kunitengeneza. Asubuhi mtoto akaja akaniambia ‘mama, Jirani amesema atakuchapa kofi, nikashangaa kwa nini.

Mama mkwe kuskia hivyo, akaanza kunipigia kelele. Nilikuwa nimelala kwake zaidi ya mwaka mmoja. Nyumba yangu ilikuwa imeharibika na kitanda pia sikuwa nayo. Nilikuwa na mtoto mchanga singeweza kulala naye huko,” Regina alisimulia.

Alidai kwamba mama mkwe alianza kumpigia kelele akisema kwamba amekuwa akimsumbua.

“Alisema sitalala kwa nyumba yake. Nikasema nitalala hapo hadi kijana wake atengeneze nyumba. Mama mkwe alitoka,  akaingia kwa chumba akaanza kutoa vitu zangu nje. Kuna begi nilikuwa nimeweka dawa zangu, nilikuwa nataka kumeza dawa akanishika. Alinishika, akanipiga na kuniangusha chini. Akawa ni kama anataka kunishika shingo. Kwa bahati mbaya, mkono yake iliingia kwa mdomo yangu nikamuuma. Wasichana wake waliniambia niende kwetu. Bwana yangu ako Homa Bay, alikuja akaniambia hakuna mahali naenda. Nimejaribu kuongea na bwana yangu ajenge nyumba amekataa kunisikia,” alisema.

Bi Rose alipopigiwa simu, alikanusha madai ya mke huyo wa mwanawe na kueleza ukweli wake.

“Tuachane na hiyo maneno. Nyumba iko wewe kuja tu utaona. Mbona hajatengeneza nyumba yake kama iko na shida?  Mimi nilitaka aende atengeneze nyumba yake, yeye anauma mimi na meno,” Bi Rose alieleza.

“Ata kama kitanda imeharibika, si atafuta fundi apige msumari alale. Mimi nilitaka aende kwa nyumba yake alale huko, hiyo ikaleta matatizo, alafu anauma mimi na meno. Nilienda kuchukua kitanda yangu, aende kwa nyumba yake akatengeneze alale. Wakati nilienda kuchukua hizo vitu, akachukua dawa ameze eti akufe. Mimi nikagonga hiyo dawa kwa mkono yake. Hapo ndio shida ilianza,” Mama Mkwe alisema.

Huku akijitetea, Regina alisema, “Nyumba ndiyo mbaya, na mapato yangu ni kidogo. Mimi sina uwezo kwa sababu hakuna kazi. Nimelala kwa mama mkwe mwaka mmoja na miezi nane. Nimeambia mume wangu, yeye hasikii maneno.”

Aliongeza, “Nilitaka kuomba mama mkwe msamaha ata kama natoka, niende kama roho imetulia.”

Bi Rose alisema, “Hiyo maneno anasema ni uongo tu. Ata saai hayuko nyumbani, sijui analala wapi. Ameniacha hapa na Watoto.”

Regina alisema tayari amemsamehe mama mkwe na akaomba pia naye amsamehe.

Bi Rose alisema ,”Sina maneno, mume wake alishasema aende nyumbani atamfuata waongee na mama yake huko. Hapo ndio anajua kama atamrejesha. Mimi sina maneno nay eye. Aende tu nyumbani, mume wake atamfuata.”

Je, una maoni ama ushauri kuhusu Patanisho ya leo?



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved