Kennedy wa miaka 30 kutoka Makueni ameomba kupatanishwa na baba mkwe ambaye amesema kwamba mahusiano yao yaliharibika baada ya yeye kukosa kulipa mahari kama walivyokuwa wamekubaliana.
Kulingana na Kennedy baba mkwe kwa jina Kivisu amekuwa akikosa kupokea simu yake tangu kukosa kupeleka mahari. Kennedy amesema kwamba, alikosa kupeleka mahari kwa kuwa kulingana na mila ya jamii ya Akamba, mtoto mvulana hawezi kupeleka mahari kwa wazazi wa mke wake ikiwa mama mzazi hajalipiwa.
“Tulikuwa na agano la kulipa mahari mwezi wa nne lakini sikupeleka kwa sababu mama wangu mzazi alikuwa hajalipiwa mahari.” Alisema Kennedy.
Akielezea kesi yake, Kennedy alisema kwamba sasa yuko tayari kulipa mahari kwa wazazi wa mke wake baada ya mahari ya mama yake kulipwa akipania kutejkeleza shughuli hiyo mwezi wa nne mwaka ujao’
Aidjha kwa upande wa baba mkwe wake, alisema kwamba amechoka na uongo wa Kennedy kwani alikosa kutimiza ahadi waliokuwa wamekubaliana. Baba mkwe, kwa jina Kibisu alisema kwamba Kennedy amekuwa na mkora na kamwe hatukata kusikia kutoka kwake. Vile vile, Kibisu alisema kwamba mtoto wa Kennedy na binti wake yuko nyumabni kwake na Kennedy hana ufahamu wa jinsi mtoto anaishi.
Mbali ya kumshutumu kuwa mkora, Kibisu alifichua kwamba Kennedy amekuwa akimtishia mwanawe kuwa angalimtoa shingo. Kibisu alisema kwamba mtoto wake alimshtaki Kennedy kwa polisi kwa vitisho vya kumuua.
Kibisu alisema kwamba tangu Kennedy kuanza kuishi na mtoto wake kabla ya kuondoka, alikuwa hajawai kufika nyumbani kwake licha ya kuishi na hata kuzaa mtoto na binti wake.
Simulizi ya Kibisu, ilibaini kwamba Kennedy alimpachika mwanawe mimba akiwa shuleni huku akipoteza pesa zake kupitia karo aliyokuwa amelipa shuleni.
“Huyo mtu ana makosa mingi, hajui kwangu, alichukua msichana akiwa anasoma, msichana akawacha school fees kwa shule, mtoto alipotea wakati walikuwa wamefunga shule.” Alisema Kibisu.
Hata hivyo Kennedy alikiri kumtishia binti wa Kibisu kuwa angalimuua ila aliomba msamaha kwa Kibisu akisema kuwa hilo halitajirudia.
“Baba Doreen mimi nilikuwa nataka nikuombe msamaha kwa vile nilikudanganya, sitawai rudia tena. Msichana alinituma niongee na wewe kwa hivyo naomba msamaha ndio tujue vile tutafanya tafadhali.” Alisema Kennedy.
Katika maneno ya mwisho, Baba mkwe alimwarifu Kennedy kuwa
kwa upande hana tatizo ila lazima azungumze na mwanawe kisha wakielewana waende
nyumbani kumwona ili kuelewana zaidi.