Cosmas ameomba kupatanishwa na mke wake kwa jina Celestine ambaye amedai kwamba walikosana kutokana na ukosefu wa maelewano katika ndoa yao. Wanandoa hawa, wameoana kwa zaidi ya miaka 10 na kubarikiwa na watoto wawili.
Kwa mujibu wa Cosmas, amekosa kumwelewa mke wake kwa kuwa na mambo mengi ambayo sababu anazozitoa zinakosa kueleweka. Wawili hao walikosana wiki mbili zilizopita, baada ya Celestine kuondoka chumbani wanakolala na mumewe na kuhamia katika chumba cha watoto bila ya kumweleza mumewe sababu haswa ya kuwacha kulala katika kitanda chao cha ndoa.
Cosmas, aidha amesema kwamba amejaribu kumhamasisha ili kufahamu kiini haswa cha mkewe kuondoka chumbani kwao ila Celestine hazungumzi.
Cosmas alimshutumu mkewe kwamba amekuwa akizungumza maswala ya familia kwa watu wa nje badala ya kumweleza wakati kuna tatizo katika ndoa yao.
Kwa upande wa Celestine, alimshtumu mumewe kwa kumpiga na hata kumtishia kumtoa shingo huku akimwambia anakosa adabu. Celestine aliomba muda wa miaka miwili ilikutafakari ikiwa angeridhia kurejea kwa Cosmas au la.
“Anipatie muda wa miaka miwili niangalie kama nitarudi ama sitarudi. Alinipiga sana akaniambia sina adabu. Aliniambia atanipiga anitoe shingo.” Alisema Celestine.
Katika kuomba msamaha kwa Celestine, Cosmas alikiri kwamba ana mtoto mchanga wa miaka mitatu ambaye alihitaji malezi ya mama. Vile vile, Cosmas alisema watoto wake wakubwa ni wa kike, hivyo basi malezi ya mama yangekuwa muhimu jambo lililomfanya kumtaka mkewe kurejea nyumbani.
Hata hivyo, Cosmas alikiri kuwa aliwahi kumpiga mkewe kutokana na hasira aliyokuwa nayo baada ya kujaribu kumbembeleza mkewe kuelezea sababu ya kuhama kutoka chumbani kwao hadi chumba cha watoto. Kwa mujibu wa Cosmas, Mkewe alitoka nje usiku wa manane, huku Cosmas akihofia kuwa angakuimwa na nyoka, basi yeye ndio angaliwajibika.
“Nilijaribu kumbeleza karibu saa nne na huzungmzi. Alitoka nje usiku angaliumwa na nyoka nani ataulizwa. Hasira zilinipanda sana.” Alisema Cosmas.
Juhudi za kumtaka Celestine kulegeza masharti yake ya kuchukua miaka miwili kufikiria ikiwa angalirejea kwa Cosmas zilikosa kufua dafu huku akisisitiza kwamba mumewe amtafute mwanamke ambaye anadhania ana adabu kumliko.
“Kila mmoja afuate shughuli zake, nipo nyumbani napumzika kabisa. Alisema
sina adabu, atafute mke mwingine mwenye adabu waishi kwa amani.”
Alisema Celestine.
Hata hivyo, Cosmas alisema ni sawa kwa muda ambao
Celestine aliamua wa miaka miwili kuwazia swala la kurejea kwake, akiahidi kuwa
atafanya mazungumzo na wawazi wake(Celestine) ili kushauriwa.