Askari wa huduma ya vijana kwa taifa Paul, ameomba kupatanishwa na mpenzi wake kwa jina Yvonne ambaye walipatana katika kambi ya NYS. Kulingana na Paul, alikosana na Yvonne mwaka wa 2022 wakati Yvonne alimpata akizungumza na msichana mwingine aliyemtambulisha kama Mary.
Paul amekiri kwamba, alikuwa anamtembelea Mary katika sehemu ya kazi aliyokuwa amepelekwa.
Paul amesema kwamba, baada ya Yvonne kumpata akiwa na Mary, alikasirika na kupelekea kuachana kwao. Baadaye, Paul aliomba msamaha kwa Yvonne na akakubali kumsameheila anashuku kwamba bado kitendo alichofanya bado kinamkera. Paul amesema kwamba, wakati mwingine akimpigia simu huwa hapokei jambo ambalo hudhania bado ana hasira.
Katika patanisho, Paul amemweleza Yvonne kwamba anaomba msamaha kwa yote yaliyotukia.
Kwa upande wa Yvonne, alimtaka Paul kumpigia pembeni ili wazungumze akihofia kwamba baba yake huskiza Radio Jambo.
“Mimi naomba msamaha kwa yote ambayo nilifanya kwa maana mimi nakupenda, I Promise.” Alisema Paul.
Aidha Yvonne, aliashiria kuogopa kurudiana na Paul akieleza kwamba Paul alikuwa tayari na mahusiano na mwanamke mwingine.
“Tutaongea tu na yeye lakini mambo ya mapenzi itakuwa ngumu, utakuwaje na mwanamke mwingine na bado unanitaka?” Aliuliza Yvonne.
Hata hivyo, Yvonne aliahidi kumpigia Paul ili wawe na mazungumzo kuhusu uhusiano wao akimwomba asimpeleke tena kwenye patanisho akikiri kwamba kitengo hicho huwa cha jamii ya Waluhya.
“Anipigie asinipeleke tena patanisho, hii patanisho inakuwanga ya waluhya.” Yvonne alissema.
Kwa maneno ya mwisho baina ya wawili hao, Yvonne alisema kwamba anafahamu kwamba wakati mwingine changamoto hutokea lakini kitu alichofanya Paul hakikukuwa kizuri akiahidi atampigia simu wazungumze.
Kwa upande wa Paul alimweleza Yvonne kwamba anampenda na kuna uwezo wa kusuluhisha changamoto zilizoko.
“Yvonne, mimi nakupenda, si ata wewe unajua nilikuwa nakupenda,
tunaweza kutatua matatizo baina yetu.” Paul alisema.