Jamaa aliyejitambulisha kama Eric Muli ,25, kutoka Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Judy Mutheu ,22, ambaye alikosana naye mwaka jana.
Eric alisema mahusiano yao ya miaka sita yalisambaratika miezi minne iliyopita ila hakujua chanzo cha hayo.
"Tulikuwa tumekaa kwa miaka sita. Miezi minne iliyopita aakanza kuwa hivi hivi. Nikimpigia simu hashiki, nikimtext hajibu. Hakuna kitu nilimfanyia. Tulikuwa tunaishi pamoja lakini nikaenda mbali kidogo, nikakuja Rongai akabaki nyumbani. Nilikuwa nashughulikia mahitaji lakini sikuwa nimemuoa," Eric alisema.
Judy alipopigiwa simu alibainisha kwamba pia yeye hajui tatizo ni nini.
"Mi sijui, si wewe ndiye ulinyamaza. Mimi sijui," alisema.
Eric alimwambia, "Kama nilikukosea naomba unisamehe."
Judy pia alitupilia mbali madai ya Eric kumtafuta na akamwagiza ampigie simu wazungumze zaidi.
"Hajawahi kunipigia simu. Kama anataka kuzungumza na mimi anipigie. Huwa hanipigii simu," Judy alisema.
Eric alisema, "Nilikuwa nampigia hakuwa anashika. Pia text hakuwa anajibu. Nilimpigia Disemba."
Patanisho hiyo haikuweza kuendelea kwani Judy alitaka kuzungumza na mpenziwe faraghani.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?