Mwanadada aliyejitambulisha kama Mary Kemunto (22) kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Joseph Mogambi (25) ambaye alikosana naye mwezi uliopita.
Kemunto alisema ndoa yake ya miaka mitano ilisambaratika Disemba baada ya kumpata mumewe akiwa na mpango wa kando.
"Tulikuwa na yeye miaka mitano. Hii Disemba ndo alianza kunicheat akaniambia ako na mpango wa kando. Nikamwambia amove on tukae na yeye, ama aendelee na mpango wa kando, akaniambia atapata siku yenye atamove on," Kemunto alisema.
"Nilimpata na mpango wa kando kwa barabara. Walikuwa wameshikana mkono. Nikamwambia nitaenda kwetu aendelee na huyo. Hiyo siku akakuja nyumbani akaniambia atamove on. Nikaenda kwetu. Juzi amenipigia simu akaniambia amemove on, nikamwambia anipee muda nijue kama nitarudi.Nataka kama amemove on na huyo msichana, ndiyo mimi nirudi. Huwa nampigia simu yake inakuwa busy," aliongeza.
Juhudi za kumpatanisha Kemunto na mumewe hata hivyo hazikufua dafu kwani kulitokea matatizo ya simu wakati Mogambi alipopigiwa.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu mahusiano ya wawili hao.