James Ambani ,28, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwewe Mama Christine (60) ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka jana.
James alisema uhusiano wake na mama mkwe uliharibika Novemba 2024 wakati ambapo alimuacha mkewe hospitalini na kutoroka.
Alidai mkewe alikuwa amekumbana na matatizo ya ujauzito ila hakuwa na uwezo wa kifedha kwa wakati.
"Tulikosana na mama mkwe. Tulipatana na msichana wa huyo mama, na tukaoana tukaenda na yeye nyumbani. Ni kama huyo mama hakufurahia. Ile wakati tulikuja na yeye nyumbani, akaanza kutafutwa," James alisimulia.
"Mwezi wa nne, akapata mimba. Mwezi wa sita ikatoka. Baada ya kutoka tukakaa na yeye nyumbani. Akapata ujauzito mara nyingine mwezi wa nane, tukaenda hospitali. Ilikuwa aende tarehe 28, tena akapata shida ya mimba kutoka hapo mwezi wa kumi na moja. Wakati huo ikatokea maneno ya kazi. Nikapigiwa simu, nikasema apelekwe hospitali Malava. Nilipata wasiwasi niikawa najiuliza kwa nini huyu msichana mimba inatoka kila saa. Nikajiuliza kwani hatukupata baraka kutoka kwa mama ama shida ni nini?," aliongeza.
James alisema ukosefu wa pesa ulimfanya akamuacha mkewe hospitalini na kutoroka, suala ambalo lilimkasirisha mama mkwe.
"Mara ya kwanza nilisaidiwa na ndugu yangu, na dada yangu. Shida ilipotokea mara ya pili nili, wakaniambia hawana pesa. Nikakaa na mke mpaka karibu saa kumi, nikapigia mamake simu nikamwambia akuje aone mtoto wake shida imetokea tena. Nilimpigia simu kama sina pesa. Madaktari walinipigia simu niende nikae na mgonjwa nikasema nakuja nimeenda kumnunulia lunch. Sikuwa na pesa, nilikuwa nahepa. Nilisema mamake anakuja. Kitu saa kumi na mbili mamake akaja. Alinipigia simu, nikakata mpaka nikazima simu. Mama mkwe alikasirika akamchukua akaenda naye nyumbani kwao. Kuna wakati msichana alikuja kwangu akavunja mlango akachukua vitu," alisimulia.
"Nataka nipatanishwe na mama mkwe. Hata kama si kurudiana na msichana, nilikuwa nataka kuomba msamaha," alisema.
Juhudi za kumpatanisha James na mama mkwe hata hivyo ziligonga mwamba kwani simu ya mama mkwe haikungia.
James aliposhauriwa kutafuta mke mwingine kwa jinsi alivyowakasirisha wakwe zakem alisema, ""Nilijaribu kutafuta mwingine lakini ndoto yangu ni kama bado iko kwa yule. Nilijaribu kuleta mwingine akatoroka,."
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?