Patrick Afuma ,56, kutoka Mumias East alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mwanawe Bonface Odwori ,32, ambaye hajakuwa na maelewano mazuri naye.
Patrick alisema mwanawe amejitenga sana na watu wengine katika familia na hajakuwa akitaka kushirikiana na wao.
"Ilikuwa ni hali ya kifamilia. Ni kijana hataki kuelezewa. Anataka kuwa kingpin, anataka kuwa yeye ndiye kusema. Mwaka jana, babu yake alimuhitaji, akakufa kama hajamuona, hakufanya vile alihitaji. Alikuja tu matanga. Babu yake ambaye amezaa mama yake alimuitisha kitu, akakosa kutimiza," Bw Patrick alisimulia.
"Mandugu zake na dada zake hataki kuelewana nao. Alisema kwamba atablock namba zetu sisi wazazi na wajomba wake. Alikuwa na bibi, wakakosana akaenda. Walikuwa na mtoto, akukaja nyumbani. Mama ya huyo mtoto alienda akapata mimba nyingine akazaa. Huwa anaskia eti huyo mama atakuja kuona mtoto wake, hataki. Akaoa msichana mwingine, akasema sisi hatujakaribisha huyo msichana nyumbani. Waliporudi Nairobi msichana akaenda. Nilitaka kujua msimamo wake kwa sababu mwezi Novemba alitwambia atablock namba zetu. Kama anataka kuishi maisha yake akuje hapa nyumbani nimpatie kipande cha shamba ajenge akae," Bw Patrick aliongeza.
Bonface alipopigiwa simu alibainisha kwamba hataki kuzungumza hewani.
"Mwambie mi niko poa," alisema kabla ya kukata simu.
Bw Patrick alijibu, "Sina shida na yeye. Yeye ndiye atanitafuta, mimi sitamtafuta. Kwetu tulizaliwa tukiwa wawili, mimi na dadangu ambaye aliaga. Nilikuwa nimechukulia watoto wangu kama ndugu zangu. Nimejihurumia sana kama kijana anaweza kufanya hivyo . Wajomba wake walimfanyia nini? Kwa upande wa Usaidizi, alikuwa ananisaidia. Nikimuitisha kitu, ananisaidia na kama hana ananieleza. Sijawahi kumpea pressure, isipokuwa ushirikiano katika familia."
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?