Michael Wambua ,23, kutoka Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Faith Wangari ,22, ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Wambua alisema uhusiano wake wa miaka mitatu uliharibika Jumapili baada ya mzozo wa kinyumbani baina yake na mpenziwe.
Alisema alipokea simu ambapo mwanaume mwingine alikuwa anampigia mpenziwe na hapo ndipo wakaanza kuzozana.
"Kuanzia mwezi wa saba mwaka jana tumekuwa tukivurugana kidogo kidogo. Jumapili mwanaume fulani akampigia simu. Mimi ndiye nilikuwa na simu nikashika. Ni kama huyo mwanaume alishtuka kuskia mimi ndiye nimeshika. Pia mimi nikataka kujua ni nani huyo. Kuingia WhatsApp nikapata amelock chat ya huyo jamaa. Nilimwambia afungue nione tukaanza kuvurugana akatoka akaenda," Wambua alisimulia.
"Nilimpigia huyo jamaa akasema yeye ni rafiki tu. Sasa hivi anasema hana uhakika kama anaweza kurudi kwangu. Nataka nijue msimamo wake. Mimi nampenda bado," aliongeza.
Faith alipopigiwa simu, Wambua alichukua fursa kumuomba msamaha mpenziwe na kumsihi warudiane.
"Nilitaka kukuuliza umeamua aje. Tumekuwa na mambo mingi lakini nilitaka kukuomba msamaha. Turudiane tuendelee na maisha. Nikikuuliza unasema kuna 10% ye kurudi. Nakupenda siwezi taka kukupoteza," alisema.
Faith alimjibu, "Ata hasira zenyewe hazijashuka ushaanza kuuliza mtu kama atarudi. Unasema tu kwa mdomo eti unapenda mtu. Mtu ataishi kulalamika. Umesahau hata mwaka jana kulikuwa na tatizo kama hili."
Wambua alidai kwamba amebadilika na akamhakikishia mpenziwe kuhusu upendo wake mkubwa kwake.
"Yeye anapenda kuinvade privacy ya mtu. Shida yake ni mtu ako insecure. Kila wakati anafikiria anacheatiwa. Kama hiyo chat alipata imelockiwa hakuthibitisha kama ilikuwa mambo ya kimapenzi. Huyo mwanaume tulikuwa tunasoma na yeye," Faith alisema.
"Mimi kwanza nataka anipee muda. Nilipata nakaa na mtu tu kwa nyumba kama mmekasirikiana. He should man up. Bado ako na utoto. Kwa saa hii siwezi jibu kama bado nampenda. Anipee muda tu. Anipee muda, ata miaka miwili. Mimi mambo na wanaume sitaki. Imagine ata anaambia vijana wengine vile amenipata na wanaume wengine," aliongeza.
Wambua alisema, "Ata mimi nilikaa chini nikaona nafaa kukomaa...Miaka miwili si atakuwa ashaenda tu."
Licha ya juhudi za Wambua kumshawishi mpenziwe, Faith alishilikia kwamba anataka muda wa kutulia pekee yake.
Katika maneno ya mwisho, Wambua alimwambia mpenziwe, "Mi nakupenda tu sana. Najuta mambo yote mabaya nimekuwa nikikufanyia. Nakumiss na nakupenda."
Faith alimwambia, "Man up. Ajiangazie."
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?