logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada aliyejifungua akiwa 15 azozana na dadake baada ya kuenda kumchukua bintiye akiwa mlevi

Martha alikiri mzozo uliibuka wakati alipomuenda bintiye akiwa mlevi chakari, na wakaanza kutupiana maneno makali na dadake.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho24 January 2025 - 08:37

Muhtasari


  • Martha alisema uhusiano wake na bwana ya dadake uliharibika kufuatia mzozo kuhusu binti yake ambaye analelewa na shemeji yake.
  • Julius aliweka wazi kwamba bado anaendelea kumlea mtoto wa Martha na akamwambia shemejiye huyo kwamba yuko huru kumchukua bintiye wakati akiweza kuimarika kifedha.


Martha Mukami ,23, kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na shemeji yake Julius Mugambi ,35, ambaye alikosana naye miaka ya nyuma.

Martha alisema uhusiano wake na bwana ya dadake uliharibika kufuatia mzozo kuhusu binti yake ambaye analelewa na shemeji yake.

"Nilimpata mtoto wangu msichana nikiwa mdogo. Nilikuwa na miaka 15. Wakati nilimpata nilimlea kidogo akafikisga miezi sita nikamuachia mama nikaenda kazi. Mamangu akaanza kuwa mgonjwa, wakampeleka hospitali ambayo sikujua. Nikisema ni kurudi nyumbani nikapata mama ashaaga," Martha alisimulia.

Martha alikiri kwamba mzozo uliibuka wakati alipomuenda binti yake akiwa mlevi chakari, na wakaanza kutupiana maneno makali na kina dadake.

"Nilipata mama amesema eti mama akae na dada yangu mkubwa mpaka wakati nitajiweza niachiwe. Mimi nilitoka kuenda kuchukua watoto. Nilienda nikiwa mlevi, pia nilikuwa naugua ile machungu ya mama. Niliwaambia wanipatie mtoto nikae na yeye. Walisema mimi ni jangili na malaya siwezi patiwa mtoto. Nilikasirika nikaanza kuwatusi. Ilifika mahali tukatupiana maneno ambayo si mazuri. Nilitoka nikaenda kwa dada yangu mkubwa kabisa nikamwambia nitaenda kabisa nisahau kama niko na mtoto. Nilitoka nikaenda nikawaacha hivyo," alisema.

"Hiyo kitu huniuma kwa sababu sasa nimekaa mpaka nikaoka, nataka turejeshe uhusiano mzuri," Martha aliongeza.

Julius alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba tayari amemsamehe shemejiye na hana shida yoyote naye.

Aidha, aliweka wazi kwamba bado anaendelea kumlea mtoto wa Martha na akamwambia shemejiye huyo kwamba yuko huru kumchukua bintiye wakati akiweza kuimarika kifedha.

"Nishamsamehe  sina ubaya na yeye hata kidogo. Mpaka saai niko na mtoto wake, ako sawa, anasoma. Hana shida kabisa. Hata nilimwambia akitaka kukuja kumuona anakuja anamchukua wanakaa na yeye. Nilimwambia nikiona amekaa vizuri atakuja amchukue mtoto wake wakae na yeye," Julius alisema.

Martha alimwambia, "Nimepiga simu juu hiyo kitu huniuma kabisa juu naona nilikosea kabisa na naona ile umoja ya kitambo iliisha. Naomba unisamehe na hiyo kitu iishe tuendelee na maisha. Nilibadilika na nikaokoka. Sasa hivi niko na mtoto mwingine kijana,"

"Mimi nimekusamehe, sina shida yoyote na wewe," Julius alimwambia.

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved