KATIKA kipindi cha Patanisho kwenye Radio Jambo, kijana mwenye umri wa miaka 23 kwa jina Moses Amadi, Mganda anayefanya kazi nchini Kenya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Rose Ojema mwenye umri wa miaka 21.
“Nilikosana na Bibi yangu on
Julai 2022 kwa sababu ya ulevi. Mke wangu alikuwa Mtu mwenye anaenda kwa baa na
kukaa huko sana na Marafiki zake hadi analala huko na saa zingine kurudi
nyumbani very late. Kwa hivi sasa niko maeneo ya Kiambu na yeye pia naskia ako
Kiambu upande ya Majani,” ujumbe wa
Amadi ulisema.
Amadi alisema kwamba ni yeye mwenyewe
aliamua kumuacha Ojema kwa sababu alikuwa akitoka na kulala nje huku akiwa
ameacha nyuma mtoto wa miezi 6.
“Mke wangu alikuwa akienda harudi
sasa nikaamua tuachane anakuja usiku nikaamua nimuache na akaenda akaniachia
mtoto akiwa na miezi 6… nikachukua mtoto nikapeleka nyumbani saizi nampigia
simu ananiambia anataka kurudi namwambia siwezi kubali….”
Baada ya kukatisha mahusiano, Amadi
alisema alimrudisha mtoto wake nyumbani kwa wazazi wake lakini sasa anataka
kurudiana na Ojema kwa sababu ya mtoto.
Mwanamume huyo alisema kuwa anataka
kurudiana na mama mtoto wake kwani sasa mtoto ana miaka 3 na ameanza kuuliza
maswali kuhusu aliko mama.
“Nataka kuongea na yeye nione
kama tunaweza sameheana… juu mtoto sasa amekuwa mkubwa anataka kuona mamake na
mimi namwambia sijui pahali alienda, sasa ana miaka 3…nataka aone mtoto na pia
tunaweza rudiana,” Amadi alisema.
Kwa upande wake, Rose Ojema alifichua
kwamba sababu ya kutorudiana na Amadi ni kwamba alioa na yeye pia akaamua
kuolewa kwingine.
“Yeye alioa na mimi pia
nikaamua kuolewa lakini sasa hivi niko nyumbani na ningependa kusikia
anasemaje,” Ojema alisema.
Baada ya wawili hao kuzungumza, Amadi
aliweka wazi nia yake kwamba angetaka warudiane na Ojema akamtaka kumpigia kwa
simu yake ili wayamalize.
Licha ya kuolewa tena, Rose Ojema
alisema baada ya ndoa hiyo kuvunjika na kurudi nyumbani, ako tayari kurudiana
na mume wa kwanza, ikiwa mume mwenyewe yuko tayari.