logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Sasa nimekuwa mzuri, jana nilipika ugali, leo nampikia mke chai!- Jamaa adai ameokoka baada ya kuombewa

Anthony alisema uhusiano wake na mzazi huyo wake umeharibika kutokana na tabia yake ya ulevi.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho12 February 2025 - 09:23

Muhtasari


  • Anthony  alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba yake Charles Nyoike (65) ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka jana.
  • Jamaa huyo alisema kwamba aliokoka baada ya watumishi wa Mungu kuzungumza naye na kumuombea.

Warangazaji

Antony Gathogo (38) kutoka Juja alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba yake Charles Nyoike (65) ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka jana.

Anthony alisema uhusiano wake na mzazi huyo wake umeharibika kutokana na tabia yake ya ulevi.

Hata hivyo, alieleza kuwa tayari amebadilika na hata kuokoka na yuko tayari kurejesha uhusiano mzuri na babake.

“Si kukosana vile lakini niko makosa mimi mwenyewe. Babangu anakuwanga mtu wa kanisa lakini nilikuwa nimeingilia mambo ya ulevi. Mwezi wa kumi na moja nikawa nimeongeza kukunywa mpaka najisahau,” Anthony alisimulia.

“Nimekuwa nikikosa kuchukua simu zake, nikichukua anaskia vile naongea anasema hataki ulevi. Nimekuwa nikiignore simu zake, nampa ahadi na sitimizi. Niliahidi kununua sikukuu, sikununua. Anapiga naangalia simu zake tu,” aliongeza.

Jamaa huyo alisema kwamba aliokoka baada ya watumishi wa Mungu kuzungumza naye na kumuombea.

“Jumatatu wiki jana nilikutana na watumishi wa Mungu na nikaokoka. Nimeokoka saa hii nasoma Bibilia. Niko na siku nane baada ya kuokoka,” alisema.

Wakati nilikuwa nakunywa, nilikuwa nasumbua bibi yangu. Kila wakati ni fujo, tunapigia baba na siwezi kuongea maongezi ambayo ni mazuri. Nilikuwa naongea ni kama ni mtu wa rika langu naongea naye,” aliongeza.

Huku akisisitiza jinsi alivyobadilika, alisema, “Niliona mambo hayaendi poa kwa sababu ata bibi alikuwa anafunga virago aende. Mke yuko ata nampikia chai. Saa hii nimekuwa mzuri, jana ni mimi nilipika ugali, leo nampikia chai, nimetoka nje nimeacha wakikunywa na watoto. Mara ya mwisho kunywa ilikuwa last Sunday but one na hiyo Jumapili jioni nikaenda kwa kanisa nikiwa mlevi sana. Nilienda tu na pombe zangu nikajipata nimeingia kanisa ambapo bibi yangu huabudu. Wakaniongelesha baada ya ibada nikamwambia askofu mashida zangu. Siku ijayo akanipea appointment. Nikaenda na nguvu za Mungu zikaniweza nikakubali kuokoka.”

Mzee Nyoike alipopigiwa simu, alibainisha jinsi amekuwa akijaribu kumuongelesha mwanawe aache ulevi ila haskii.

Pia alisikika kutilia shaka madai ya kijana huyo wake kwamba ameacha ulevi.

“Si nilimukanya yeye hataki kuskia. Tumeongea mengi kuhusu pombe. Anasumbua. Mimi namuongelesha kila wakati. Msamaha anaomba mara mingi. Yeye ni mtu wa kurudia rudia nimemzoea. Hiyo msahama ameomba mara mingi,” Mzee Nyoike alisema.

Aliongeza, ‘Nitampea miezi mbili tatu nione kama ni ukweli anaongea sababu hiyo anakwambia huwa anasema kila wakati asamehewe. Sasa tutampa probation. Mimi sina shida nay eye lakini mambo yake ni kuomba msamehe kila wakati.”

Huku akimgeukia mwanawe, alimwambia, “Sasa unaenda kusumbua hao marafiki wangu kwa nini. Hao ni marafiki zangu nawajua. Tuliachana uwachane na pombe na uache kuvuruga pombe. Wewe ni mtu ako na ujanja sana.”

Anthony alijaribu kujitetea akieleza kwamba ameamua kubadilika.

“Sijakuwa nikichukua simu zako lakini ni vile wakati huo bado nilikuwa kwa vikombe. Ningependa Kenya yote ijue nimeokoka. Naomba kila siku hata nimetoka kuomba. Aamini nimebadilika na anisaidie kwa maombi,” alisema Anthony.

Bwana Nyoike alikubali kurejesha uhusiano mzuri na mwanawe na akamsamehe.

“Mimi sina shida na yeye. Mimi niko na roho safi. Siwezi kubali akosee. Kusamehewa ni kuacha . Ata mimi kuna wakati nilikuwa mlevi na niliacha kabisa. Niliacha mambo ya kuvurugana na watu. Nimekubaliana na yeye amebadilika,” alisema.

Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved