
Jamaa aliyejitambulisha kama Jose Indeche (28) kutoka Mumias alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Sharon Iminza (24) ambaye alikosana naye miezi kadhaa iliyopita.
Jose alisema ndoa yake ya mwaka mmoja unusu ilisambaratika Desemba mwaka jana wakati mkewe alitoroka na kurudi nyumbani kwao.
Alieleza kwamba mkewe alikasirika kufuatia vurugu za kinyumbani zilizotokea wakati alirudi akiwa mlevi.
“Ilikuwa Desemba 2023 tukaenda sherehe ya vijana kunywa pombe kiasi. Nilirudi nyumbani usiku kama nimelewa, sikuwa najielewa nikaanguka kwa mboga yenye alikuwa amepika hapo. Alichelewa kufungua mlango nikausukuma nikaanguka huko kwa mboga. Akaanza kuniambia ‘Sasa tutakula nini?’. Nikamwambia anyamaze ati ni yeye hakuwa ameweka mboga vizuri. Akanipiga kofi. Nilihuzunika sana,” Jose alieleza.
“Nikijaribu kumpigia, sijui aliweka simu yangu block. Sikuwa nimeenda kwao bado, ndio maana nimewapea namba ya baba mkwe. Nikipiga baba mkwe anakuwa mkali. Nilikuwa nimeishi na huyo msichana kwa mwaka mmoja unusu. Nilikuwa nataka niongee na Sharon nimuombe msamaha kama nimekosea turudiane na yeye. Ningetaka turudiane tuweze kusaidiana,” aliongeza.
Kwa kuwa Jose alituma namba ya baba mkwe, alipigiwa simu na kufichua kwamba alikerwa na jinsi kijana huyo alimpiga bintiye.
“Huyo msichana bado hajamuoa rasmi. Mambo ya msichana siwezi jua vizuri lakini kuna kitu huyo jamaa alimfanyia sikufurahia. Alirudi usiku na akampiga. Vile alimpiga sikufurahia,” Babake Sharon alisema.
Jose alichukua fursa hiyo kuomba msamaha akidai kwamba bado anampenda sana.
“Najua niliwakosea lakini ningependa mnisamehe. Bado napenda huyo msichana. Tulibishana naye lakini nitakuja tuongee kabisa. Nitatafuta nafasi. Lazima nitafute kitu ndio nikuje huko,” alimwambia baba mkwe.
“Msichana alikuwa anasema wazazi walikufa. Hakuwa anataka nijue kwao. Alitaka nimalize kujenga kwanza,” aliongeza.
Babake Sharon alimwambia, “Utakuja vipi? wakati ukikuja
unabaki kwa gate huko. Kutoka uchukue
msichana wangu. Umewahi kuja kwangu. Hiyo mwaka moja na nusu, hukuwa unajua
njia ya kuja kwangu? Wewe jipange ukuje tuongee.”