logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Heri nife nimuachie huyo jamaa!" Jamaa alamika kwa uchungu kuhusu mke wake mjamzito ku'cheat

Geoffrey alisema amekubali kumsamehe mkewe ila akamuomba aache kuenda nje ya ndoa yao ya miaka miwili.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi25 August 2023 - 06:12

Muhtasari


  • •Esther alisema hakujakuwa na amani nyumbani tangu wiki iliyopita kwani mumewe amekuwa akimshuku kuwa na mipango wa kando.
  • •Geoffrey alisema amekubali kumsamehe mkewe ila akamuomba aache kuenda nje ya ndoa yao ya miaka miwili.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Esther Malika ,20, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Geoffrey Wamalwa ,31, ambaye amekuwa akizozana naye kwa nyumba.

Esther alisema hakujakuwa na amani nyumbani tangu wiki iliyopita kwani mumewe amekuwa akimshuku kuwa na mipango wa kando.

Alisema kuwa shida ilianza baada ya mumewe kumpata akizungumza na kijana mmoja ambaye alijaribu kumtongoza.

"Nyumbani hakujakuwa na amani. Nikitoka mzee wangu anashinda akinishuku. Nikirudi  napata amefura. Anasikia sana fitina ya watu. Ukimwambia sio hivyo anakataa," Esther alisema.

Aliongeza, "Kweli alinipata sio eti nakataa.Kuna siku mtu alikuwa amenizidikiza. Tulikutana naye tu kwa njia, nikamwambia tuongee kama tunatembea. Yeye ndiye alikuwa akijaribu kunitongoza. Nikamwambia sitaki kusimama tuongee kama tunatembea.Tulikuwa karibu kufika kwa lango na nilikuwa naona mzee wangu nikamwambia asikimbie ataniletea shida. Mume wangu akawa na hasira akataka kumchapa. Nikamwambia asimchape. Akataka tupigane lakini nikamkataza. Kuanzia hapo nyumba haikaliki. Ilikuwa mara ya kwanza tu. Ni kweli alifanya uchunguzi hadi akanipata. Sijakataa."

Esther pia alikiri kwamba aliweka password kila mahali kwenye simu yake baada ya mume wake kufunga simu yake.

Geoffrey alipopigiwa simu alifunguka kuhusu machungu yake huku akieleza jinsi mkewe amekuwa akienda nje ya ndoa.

"Mke wangu nimejaribu kumkataza mambo ya mipango ya kando lakini haskii. Mimi nilikuwa nimeamua nikufe nimuachie boma. Anasema nimsamehe alafu anarudi na huyo kijana. Huyo kijana ni mtu wa area hii na mimi nimetoka Kitale. Nimeshika yeye karibu mara mbili. Jana ilikuwa mara ya pili," alisema.

Alisema kuwa inamuuma sana mkewe akienda nje ya ndoa kwani amezaa naye mtoto mmoja na pia ana ujauzito wake wa mwezi mmoja.

"Ana uhusiano na huyo jamaa kwa zaidi ya miezi mitatu. Sijalala usiku wote. Stress inanisumbua. Nasema heri nikufe nimuachie huyo jamaa. Mimi nakufaa kwa sababu ya huyo bibi yangu. Nimeteseka sana naye katika shida na raha. Anataka apende mwingine aniache mimi," Geoffrey alisema.

Baada ya mkewe kujaribu kumuomba msamaha, Geoffrey alisema "Kwanini unataka tu nikufe? Nitakufa tu juu yako. Nitakusamehe lakini najua utakutana na huyo jamaa. Wewe ni mambo ya chatting usiku wote."

Esther hata hivyo alimuomba msamaha mumewe na kumweleza kwamba hataki kukaa na msongo wa mawazo juu yake.

Aidha, alikiri kuwa amekuwa akienda nje ya ndoa ila akabainisha kuwa haijakuwa ikiendelea kwa muda mrefu.

"Hatujakuwa kwa mahusiano kwa muda mrefu. Mimi nimeacha," alisema.

Geoffrey alisema amekubali kumsamehe mkewe ila akamuomba aache kuenda nje ya ndoa yao ya miaka miwili.

"Mama Joni. Mimi nakupenda kama mama ya watoto wangu. Mimi sitawahi kusaliti, Na wewe uache hayo maneno. Wewe ndiye umebeba roho yangu," alisema Geoffrey.

Esther alimwambia, "Jeff mimi nakuhakikishia leo nimeacha hayo mambo. Nakupenda kama njugu karanga."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved