"Nakupenda kama Radio Jambo na Lolipop!" Jamaa asherehekea baada ya kupatanishwa na mkewe

Samuel alisema ndoa yake imekosa amani tangu wakati alipompata mkewe akiwasiliana na baby daddy wake.

Muhtasari

•Samuel alisema ndoa yake ya miaka miwili imekosa amani tangu wakati alipompata mkewe akiwasiliana na baba ya mtoto wake.

•Caroline alifichua kuwa mumewe amekuwa akitishia maisha yake na hivi majuzi alimwambia aondoke kwake.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho Samuel Mokaya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wa Caroline.

Samuel alisema ndoa yake ya miaka miwili imekosa amani tangu wakati alipompata mkewe akiwasiliana na baba ya mtoto wake.

"Jumanne jioni nilichukua memory yangu nikaweka kwa simu ya mke wangu. Simu yake huwa inarekodi mazungumzo ya simu. Nilipochukua kadi yangu nilisikia mazungumzo yake na baby daddy wake. Nilisikia walichokuwa wanaongea na haikuwa kuhusu mtoto," Samuel alisimulia.

"Alikuwa anasema eti siku atatoka hapa kwangi ataenda mahali huyo mwanaume yuko waishi na pamoja," 

Samuel alikiri kuwa alisikitika sana baada ya kusikia mazungumzo hayo na akachukua hatua ya kukuabiliana na mkewe. 

"Mi niko tayari kulea mtoto wake ata kama baba wa huyo huwa hamsaidii" Alisema.

Caroline alieleza kwamba mumewe amekuwa akiyatoa maneno yao ya ndani nje, jambo ambalo limekuwa likimkera.

Pia alifichua kuwa mumewe amekuwa akitishia maisha yake na hivi majuzi alimwambia aondoke kwake licha ya kuwa tayari walikuwa wamesuluhisha mzozo wake.

"Ilifika mahali ukaniambia nitoke kwa nyumba yako niende. Nilikwambia tuzungumze hayo yaishe lakini wewe mwenyewe ulitoka ukaenda kutangaza huko nje," Alisema

Gidi alifanikiwa kuwapatanisha wawili hao na wakakubaliana kwamba watakuwa wanasuluhisha mizozo yao kwa pamoja.

"Nakupenda kama Radio Jambo na Lollipop" Samuel alimwambia mkewe.

Caroline alisema,"Asiwahi kunikosea tena. Kama nimekosea akae chini aniulize nini kimetokea tusuluhishe"