Patanisho: "Alishaoa mke mwingine lakini ningependa kurudi " Mwanadada aomba mumewe amchukue tena

Muhtasari

•Cynthia alisema aligura ndoa yake ya miaka ya mitatu mwezi Machi mwaka jana baada ya mumewe kumchapa.

•Mugo alidai kuwa Cynthia alileta mzaha katika ndoa yao ndiposa akaamua kusaka mke mwingine.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi mwanadada aliyejitambulisha kama Cynthia alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mume wake Andrew Mugo. 

Cynthia alisema aligura ndoa yake ya miaka ya mitatu mwezi Machi mwaka jana baada ya mumewe kumchapa.

Alikiri kuwa mumewe alimchapa baada yake kumtupia cheche za maneno alipokataa kumpatia pesa za kutengeneza nywele.

"Nilikuwa nimemtusi alafu akanipiga vibaya. Vile nilipona babu yangu akaaga nikaenda matanga, sikurudi. Nilimwambia anikujie huko akakataa..  Alikuwa amekataa kunipatia pesa ya kutengeneza nyweke nikamtusi," Cynthia alisimulia.

Mwanadada huyo alifichua kuwa mumewe tayari ameoa mke mwingine ila akasisitiza kuwa bado angependa kurudi.

"Alishaoa lakini ningependa kurudi huko. Mtoto siishi na yeye, ako naye," Alisema.

Mugo alipopigiwa simu alidai kuwa Cynthia alileta mzaha katika ndoa yao ndiposa akaamua kusaka mke mwingine.

Alisema tayari alikuwa amechokeshwa na tabia za Cynthia kwani yeye alitaka mwanamke mwenye msimamo.

"Mimi niko na mke mwingine. Huyo ni kama hayuko serious na ndoa. Siwezi kushinda nikifanya hiyo biashara kila wakati. Roho yangu ilichoka kabisa," Alisema.

Cynthia alipoomba kurudi Mugo alijibu,"Na mwenye ako kwa nyumba ataenda wapi? Ulikataa kuja sasa nitafanya vipi,"

Mugo alieleza kuwa mke wake wa sasa tayari alikuwa amekubali Cynthia arudi waishi pamoja ila yeye mwenyewe akakataa.

Alifichua kuwa Cynthia alikuwa amekatiza mawasiliano yao kwa kumblock kwa simu. Hata hivyo alikubali kukutana na mama huyo wa mtoto wake ili wajadiliane zaidi kuhusu kurudiana.

"Tafuta nafasi Jumapili ili tuongee," Alimwambia.