Patanisho: "Ameniwaste! Amenipea stress!" Mwanadada alalamika kwa uchungu baada ya mpenziwe kumkataa

"Nimeshtuka sana. Nilimwambia sitaki stori zake. Siko tayari sasa hivi," Jonathan alisema.

Muhtasari

•Moraa alisema mahusiano yao ya mwaka mmoja yalivurugika wakati mpenzi wake alipompigia simu akakosa kushika.

•Moraa alisema, "Angeniambia mapema, ameniwaste. Amenipea stress.. Sina neno naweza kumwambia."

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Mwanadada Rose Moraa ,21, kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Jonathan ,21, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Moraa alisema mahusiano yao ya mwaka mmoja yalivurugika wakati mpenzi wake alipompigia simu akakosa kushika.

"Ilikuwa Ijumaa asubuhi saa mbili. Mimi sikuwa karibu na simu, nikakuja nikapata missed call. Kumpigia hakuchukua. Nikamwandikia ujumbe nikamuuliza shida ni nini akasema hataki mambo yangu ashamove on. Alisema ameamua hivyo tu sijafanya kosa lolote. Mimi niko serious, yeye ndiye sijui," Moraa alisema.

Moraa alisema amekuwa akijaribu kumpigia simu mpenziwe lakini hajakuwa akichukua.

Jonathan alipopigiwa simu mwanzoni alikana kumjua Moraa kabla ya baadaye kumbainishia kuwa hataki mambo yake.

"Nilikwambia acha nitulie kiasi kwanza. Nilikwambia hujanikosea mahali lakini hatuwezi,"  Jonathan alisema.

Moraa alijaribu kumshawishi kwa kumhakikishia kuwa bado anampenda sana ila maneno yake yaliangukia masikio yaliyotiwa pamba.

"Nimeshtuka sana.. Nilimwambia sitaki stori zake. Siko tayari sasa hivi," Jonathan alisema.

Moraa alisema, "Angeniambia mapema, ameniwaste. Amenipea stress.. Sina neno naweza kumwambia."

Kwa kumalizia, Jonathan alimwambia Moraa, "I think umesikia the reason why. That is it!"

Je, maoni yako ni yepi kuhusu Patanisho ya leo?