Patanisho: Denno ahuzunika baada ya kuachwa, kublockiwa na mpenzi aliyekaa naye mwezi mmoja

Alidai kuwa anashuku huenda mpenzi huyo wake alikuwa mjamzito wakati alipotoroka

Muhtasari

•Denno alisema Shiru alikaa naye kwa mwezi mmoja kabla ya kuomba kuenda nyumbani kwao ila hakuwahi kurudi.

•Denno alieleza kwamba alikaa na Shiru kati ya Octoba na Novemba mwaka jana kabla ya mahusiano yao kusambaratika.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Denno ,24, kutoka Meru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Shiru ,20, ambaye alikosana naye mwaka jana.

Denno alisema Shiru alikaa naye kwa mwezi mmoja kabla ya kuomba kuenda nyumbani kwao ila hakuwahi kurudi.

Shiru tulipatana na yeye Nairobi mwaka wa 2022. Tukakaa na yeye. Akaniambia anataka tuende Meru na tukakuja," Denno alisimulia.

Aliendelea, "Aliniambia anataka kutembea nyumbani nikamwambia ni sawa akaenda. Tukawa tunaongea kwa simu. Ilifika mahali akaniambia nisimpigie simu ati ameolewa na mtu mwingine. Saa hii nikimpigia simu ameniweka blacklist."

Denno alieleza kwamba alikaa na Shiru kati ya Octoba na Novemba mwaka jana kabla ya mahusiano yao kusambaratika.

Alidai kuwa anashuku huenda mpenzi huyo wake alikuwa mjamzito wakati alipotoroka kwani alimwambia anaweza kulea mtoto pekee yake.

"Nilikuwa naona  ni kama alikuwa na mimba. Alikuwa ameniambia nisimtafute ameolewa. Nilitaka kujua kama ako na mtoto wangu. Nilikuwa naona dalili za mimba," alisema.

Juhudi za kuwapatanisha wawili hao hata hivyo hazikufua dafu kwani simu ya Shiru haikuingia licha ya Ghost kupiga mara mbili.

Je, ushauri wako kwa  Denno ni upi?