Patanisho: Jamaa aachwa baada ya kumkataza mkewe wa miaka 10 kuzungumza na single mothers

Wambua alimshtumu mkewe kwa kuwa kichwa ngumu na kuchochewa na kina mama wasio na waume.

Muhtasari

•Wambua alisema ndoa yake ya miaka kumi ilivunjika Januari mwaka huu wakati mkewe alipotoroka pamoja na watoto wao.

•Catherine alifichua kuwa Wambua hajawahi kujitambulisha rasmi nyumbani kwao wala kupeleka mahari.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Paul Wambua ,40, kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Catherine Mutheu ,37, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Wambua alisema ndoa yake ya miaka kumi ilivunjika Januari mwaka huu wakati mkewe alipotoroka pamoja na watoto wao.

Alimshtumu mkewe kwa kuwa kichwa ngumu na kuchochewa na kina mama wasio na waume.

"Bibi yangu alianza kuwa kichwa ngumu juu ya kushinda na single mothers. Wengine wao hawana tabia nzuri. Nilijaribu kumuonya haskii. Ikafika mahali tukakosana. Wakati shule zilifunguliwa hakuwapeleka. Kumbe alikuwa na njama ya kuenda kwao na sikujua," Wambua alisema.

Aliongeza, "Tulikuwa tumekosana hapo tukiruka mwaka, Tukaongea nikamwambia hiyo stori imeisha. Nikaona haniongeleshi ni kama namlazimisha kuniongelesha.

Baada ya kuenda nilijaribu kumtafuta na kumpigia simu ikawa haingii. Nilikuwa nimemuoa lakini sikuwa nimepeleka mahari. Nilienda kwao lakini watu wao wakanionyesha madharau. Sijui waliona nikiwa chini ama waliona aje."

Catherine alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hataki kurudiana na mzazi huyo mwenzake.

Aidha, alifichua kuwa Wambua hajawahi kujitambulisha rasmi nyumbani kwao wala kupeleka mahari.

"Mwambie sirudi. Tumekaa miaka kumi. Hata hajawahi kusema yeye ndiye ako na mimi. Hajapeleka mahari, hata hajakanyaga huko," Catherine alisema.

Aliongeza, "Sitaki ndoa yake. Nilimwambia aoe. Mimi sitaki mambo ya ndoa. Aliniambia ata nikienda siku tatu atapata mke mwingine na aoe.

Nilikuwa navumilia tu kwa sababu nilitaka ndoa. Saa hii sitaki ndoa yake. Nitalea watoto wangu wawili. Sitaki mwanaume nimechoka."

Huku akijitetea kuhusu sababu yake ya kutojitambulisha kwa kina mkewe, Wambua alisema, "Mimi nimesumbuliwa na tumbo miaka kama saba. Ata yeye anajua. Nimekuwa nikimtafutia na hiyo shida, Sasa ndo anaona sifai."

Wawili hao kwa bahati mbaya hawakuweza kupatana kwani Catherine alishikilia uamuzi wake wa kutotaka ndoa.

Je, una ushauri gani kwa wawili hao?