Patanisho: Jamaa aachwa msimu wa Krismasi baada ya kumuambia mkewe "tumia akili"

Njoroge alisema mkewe alimuarifu kuwa anapanga kwenda kufanya kazi Qatar.

Muhtasari

•Njoroge alisema kuwa aligombana na mama huyo wa mtoto wao mmoja na kimzaha tu akamwambia atumie akili.

•Maryanne alipopigiwa simu alimuambia Njoroge apige hatua ya kuenda nyumbani kwao ili waweze kusuluhisha.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

James Njoroge ,35, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Maryanne Njeri ambaye alitoroka mwezi Desemba

Njoroge alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka mitano takriban siku tatu kabla ya Krismasi kufuatia matatizo ya mawasiliano.

Alisema kuwa aligombana na mama huyo wa mtoto wao mmoja na kimzaha tu akamwambia atumie akili.

"Vile nilimuambia mke "atumie akili akifanya mambo yake" alichukulia kama ni matusi na akatoroka," alisema.

Alisema kuwa baadaye alipozungumza na Maryanne alimuarifu kuwa anapanga kwenda kufanya kazi Qatar.

"Aliniambia anataka kuenda Qatar aachie mamake mtoto. Mwishoni wa mwaka jana alikuwa ameniambia anataka kuenda kazi huko," alisema.

Njoroge alisema juhudi za kutatua mzozo wao hazijafanikiwa kwani mkewe amekuwa akikata simu zake.

"Dadake mkubwa alisema ata yeye hamuelewi  kabisa," alisema.

Maryanne alipopigiwa simu alimuambia Njoroge apige hatua ya kuenda nyumbani kwao ili waweze kusuluhisha.

"Si nilikwambia ukuje nyumbani," alimwambia kabla ya simu kukatika.

Njoroge alisema kwamba atafuatilia zaidi na kuenda kwa kina Maryanne.