logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Sina muda na yeye, anisahau kabisa!" Mwanadada amkataa mumewe

•Shikuku alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka moja wiki jana baada ya wao kuhusika katika mzozo wa nyumbani. •Catherine hakuficha hasira yake dhidi ya mumewe na akaweka wazi kuwa hakutaka kuzungumza naye.

image
na Radio Jambo

Makala29 September 2022 - 05:24

Muhtasari


•Shikuku alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka moja wiki jana baada ya wao kuhusika katika mzozo wa nyumbani.

•Catherine hakuficha hasira yake dhidi ya mumewe na akaweka wazi kuwa hakutaka kuzungumza naye.

Ghost na Gidi

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, Leonard Shikuku (28) alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Catherine (22).

Shikuku alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka moja wiki jana baada ya wao kuhusika katika mzozo wa nyumbani.

"Wiki jana aliniambia anataka kuenda nyumbani kwao. Kwa kuwa mfuko yangu ilikuwa chini nikamwambia ataenda siku ingine. Tulivurugana kwa muda alafu nikamchapa kofi kidogo," alisema.

Shikuku alisema baada ya kumpiga mkewe alikasirika na kutoroka nyumbani kwao.

"Alienda pekee yake alafu akatumana mtoto akujiwe. Sasa hivi nikipiga simu ananiongelesha kwa madharau,"

Catherine alipopigiwa simu hakuficha hasira yake dhidi ya mumewe na akaweka wazi kuwa hakutaka kuzungumza naye.

"Sina muda na yeye. Anisahau kabisa!" alisema kabla ya kukata simu.

Shikuku alipopatiwa fursa ya kuomba msamaha hewani alimuomba mkewe kuelewa sababu yake kutompatia nauli ya kuenda kwao.

"Wakati mwingine mtu anaweza kuwa hana kile unataka lakini ana nia ya kusaidia. Nisamehe tu na turudiane tulee mtoto wetu," alisema.

Gidi na Ghost walimshauri ampatie mkewe muda wa kupunguza hasira.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved