Patanisho:Mwanadada atishia kujitoa uhai ikiwa jamaa aliyedai kumpenda na wanawe hayuko serious naye

"Roho yangu iko kwake sana. Kama ako serious aniambie, kama hako serious naweza chukua maisha yangu kabisa," Emma alisema.

Muhtasari

•Emma alisema amekuwa kwenye  mahusiano yasio wazi na Collins kwa miaka mitano na alitaka kujua msimamo wake.

•Emma alidai kwamba jamaa huyo amekuwa akiwasaidia watoto wake wawili hata kama hakuwazaa naye.

Image: RADIO JAMBO

Mwanadada aliyejitambulisha kama Emma Akinyi (20) kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Collins Otieno (26).

Emma alisema amekuwa kwenye  mahusiano yasio wazi na Collins kwa miaka mitano na alitaka kujua msimamo wake.

Aidha, alifichua kwamba ana watoto wawili ambao hakupata na Collins. Hata hivyo, alidai kuwa jamaa huyo anawapenda.

"Niliolewa nikiwa na miaka 15. Nilifanya KCPE nikiwa na miaka 14, nilipata mimba nikaenda kwa shangazi yangu nikazalia huko. Huko ndo tulijuliana na huyo kijana. Baada ya muda aliniambia tuende naye Nairobi. Baada ya miezi miwili tu aliniambia anaenda kazi Isiolo akasema nikuje nyumbani atanikujia," Emma alisimulia.

Aliongeza, "Mimba ya pili si yake lakini nilimuelezea tu. Hakukasirika aliniambia nimtumie picha ya mtoto WhatsApp. Mimba ya kwanza si yake na ya pili si yake. Tulijuana naye 2016 baada ya kuzaa mtoto wa kwanza.  Tunaongea naye  vizuri anasema atakuja nyumbani tu. Huwa anauliza nitafanya biashara gani akasema atatuma pesa akipata.. Nikimpigia simu yeye huwa anasema wameenda KDF mission huko Somali, Isiolo, Garissa. Kwa hivi sasa mimi niko Kisumu na yeye ako Nairobi. "

Collins alipopigiwa simu aliweka wazi kuwa tayari amezungumza na mwanadada huyo na akaahidi kuongea naye zaidi baadae.

"Nimeongea na yeye saa hii.. Si tumeongea. Nitakupigia tubonge, Anipigie tutaongea," Collins alisema.

Emma akiri alizungumza na mpenzi huyo wake asubuhi ila hakuwa wazi kwenye mazungumzo yao, "Alisema tutaongea akitoka kazi. Ameniambia nikuwa tu mpole atanipigia simu aniambie vile kuko."

Alidai kwamba jamaa huyo amekuwa akiwasaidia watoto wake wawili hata kama hakuwazaa naye.

"Nilipomwambia mtoto huyo mdogo ni mgonjwa alinitumia 5,000. Sina mtoto wake lakini anawapenda. Huwa anawasaidia mara moja moja," alisema.

Emma aliweka wazi kuwa moyo wake umekwama kwa Collins na hata kutishia kujitoa uhai ikiwa jamaa huyo hana hisia sawa.

"Roho yangu iko kwake sana. Kama ako serious aniambie lakini kama hako serious na mimi chenye anataka atapata tu,, Naweza chukua maisha yangu kabisa," alisema.

Gidi hata hivyo alimpatia ushauri maalum dhidi ya kuchukua hatua hiyo, "Una miaka 20. Bado uko na miaka mingi. Kama mtu amekataa kucommit miaka 5 ishara anakutumia tu. Hataki kukuambia ukweli wa mambo. Wacha kuweka imani yako kwa mwanaume hajacommit miaka 5. Usiwahi kujilazimisha kwa mwanaume. Mwanamke kama anakupenda atakutafuta tu. Kama anakutumia atakuzungusha tu."