(Video) "Nilishaolewa kwingine, yeye ni fullstop!" Mwanadada amkataa katakata aliyekuwa mumewe

"Sina muda naye, tayari nimeolewa kwingine!" Mwanadada huyo alisema.

Muhtasari

•Alex alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka saba mwezi Aprili kufuatia malumbano mengi kati yao.

•Ili  kumthibitishia Alex kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake, Milka alimkabidhi mume wake wa sasa simu ili awasiliane naye.

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Alex alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Milka.

Alex alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka saba mwezi Aprili kufuatia malumbano mengi kati yao. Alifichua kwamba tayari alikuwa amepata mtoto mmoja na Milka.

Alex alifichua kuwa mkewe alizozana naye kuhusu ulevi wake miongoni mwa mambo mengine mengi ambayo alishindwa kueleza.

Alisema kwa sasa anakumbwa na msongo wa mawazo huku akieleza jinsi anavyompenda mke huyo wake.

Milka hata hivyo alipopigiwa simu alisema hawezi kurudiana na jamaa huyo wa tayari huku akiweka wazi kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake. 

Alex hata hivyo alieleza kuwa itakuwa ngumu kwake kukubali kumsahau mkewe na kutafuta mwingine.

Ili  kumthibitishia Alex kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake, Milka alimkabidhi mume wake wa sasa simu ili awasiliane naye.

Tazama video ili kufuatilia yote yaliyojiri katika kipindi hicho:-