(Video) Patanisho: Mwanadada mjamzito abubujikwa na machozi akisimulia masaibu ya ndoa yake

Faith alishindwa kushikilia machozi baada ya kusimulia kisa chake cha kihisia.

Muhtasari

•Faith alisema aligura ndoa yake ya miaka mitatu baada ya kushuku mumewe kwa kuwa na mahusiano ya nje.

• Faith alishindwa kuvumilia ndoa yake na kurudi kwao ila wazazi wake wakakosa  kumpokea vizuri.

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi, kitengo cha Patanisho, mwanadada aliyejitambulisha kama Faith alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Levis Ndori.

Faith alisema aligura ndoa yake ya miaka mitatu baada ya kushuku mumewe kwa kuwa na mahusiano ya nje.

Alidai kwamba alipata mipira ya kondomu kwenye mfuko wa nguo ya mumewe na alipochukua hatua ya kumhoji akawa mkali kwake.

"Nilipata mipira ya kondomu kwa mifuko yake. Vile nilimuuliza akaona mbaya. Aliniambia kama sitaweza kustahimili niende kwetu," Faith alisimulia.

Kutokana na hayo Faith alishindwa kuvumilia ndoa yake na kurudi kwao ila wazazi wake wakakosa  kumpokea vizuri.

"Nikimpigia simu sasa huwa ananiambia hata nikirudi bado nitapata mipira ya kondomu na itabidi nivumilie. Wazazi wananiambia nirudi tu nivumilie ama nirudishe mtoto," Alisema.

"Ni kama aliwashinda wazazi wake kwa sababu waliniambia huwa hawasikilizi. Hawasikizi hata dada zake... Nilimpigia simu msichana mwingine akashika.Msichana huyo aliniambia ni mfanyikazi mwenzake," 

Juhudi za kumfikia Levis ziliangulia patupu kwani alikosa kushika simu yake licha ya Gidi kufanya majaribio mengi.

Faith ambaye alisikika mwenye uchungu mwingi aliendelea kufunguka mengi kuhusu masaibu yaliyokumba ndoa yake.

"Nyumbani hakuna mahali nakaa. Alinioa baada ya kunipachika ujauzito wa kwanza. Wakati wazazi walianza kunipeleka mbio alikuja akauliza kama naweza kuishi na yeye. Wakati nilienda kwake alianza kubadilika"

Aliongeza "Niko na ujauzito wa miezi mitatu. Naogopa kwa sababu naambiwa na mabinamu wake nitoe ujauzito. Mara ya kwanza nilijifungua kwa njia ya upasuaji."

Faith alishindwa kushikilia machozi baada ya kusimulia kisa chake cha kihisia.

Je, ushauri wako kwa mwanadada huyo?