Mpenzi wangu anajua nafanya kazi kwa 'supermarket' lakini nafanya kwa chumba cha kuhifadhi maiti-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Mwanamume aeleza kazi anayofanya kinyume ya yale mpenzi wake anajua
  • Mwanamume huyo alifichua kwamba anafanya kazi katika chumba cha kuhifadhi maiti lakini mpenzi wake anajua anafanya kazi kwa supermarket 
Teke Teke:Mbusi na Lion
Image: Studio

Katika kipindi cha toboa siri kwenye radiojambo, siku ya Jumatatu mwanamume mmoja aliwashangaza wengi baada ya ufichua kazi ambayo anafanya kinyume ya yale mpenzi wake anajua.

Kwa kweli lazima kila mtu afanye juu chini ili apate riziki ya kila siku na kuweka chakula mezani mwake.

Lakini kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kufanya kazi fulani kwa maana wamesoma na wamehitimu na shahada kuto kwenye chuo kikuu.

Pia kuna watu ambao wanakataa kazi fulani kwa ajili ya wapenzi wao.

Huu hapa usimulizi wake;

"Ninafanya kazi katika chumba cha kuhifadhi maiti, lakini mpenzi wangu anajua kwamba nafafanya kazi kwa duka kubwa yaani supermarket

nimeamua kutoboa siri kwa maana anakuja mwezi ujao kuishi na mimi, huwa nafanya kazi yangu usiku alafu natoka mchana

Huwa naosha maiti, nataka ajue kutoka leo kwa maana nampenda sana, sijui kama ataniacha baada ya kusikia haya au atazidi kunipenda." Alieleza Mwanamume huyo.

Je mpenzi wako anafahamu unafanya kazi gani, na unaweza kuacha kufanya kazi kwa ajili mpenzi wako hapendi kazi hiyo?