Nilipeleka 'boxer' yangu kwa mganga ili nisiwahi kosa kazi-Mwanamume amtobolea mkewe siri

Muhtasari
  • Mwanamume atoboa siri jinsi alipeleka 'Boxer' kwa mganga

Katika kipindi cha mbusi na lion teketeke, mwanamume mmoja alimtobolea mkewe siri kuhusu 'boxer' yake na jinsi huwa anapata kazi.

Huku akisimulia jinsi alipeleka 'boxer' yake kwa mganga ili apate kazi alisema kwamba huvaa, 'boxer' hiyo kila siku.

"Nilipeleka boxer yangu kwa mganga ili nikuwe nikipata kazi kila siku, kwa maana mimi ni mtu wa kibarua

Kuna wakati mke wangu alificha boxer hiyo na nilikuwa nikienda kutafuta kazi naambiwa hamna kazi kwa wiki nzima

Nataka kumtobolea siri kwamba boxer hiyo ambayo huwa nafua na navaa kesho yake ndio hutafuta unga wa kila siku

Mganga aliniambia ikizeeka naeza nunu ingine nimplekee, akaniwekee dawa tena, sasa nimeivalia kwa miaka miwili," Alisimulia mwanamume huyo.