Nilimpata mwalimu akiiba sukari 'staffroom'-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri na watangazaji wako uwapendao Mbusi na lion mwanamume na mwanafunzi ambaye alimaliza kidato cha nne mwaka wa 2019 alitoboa siri jinsi alimpata mwalimu akiiba sukari

Katika kitengo cha toboa siri na watangazaji wako uwapendao Mbusi na lion mwanamume na mwanafunzi ambaye alimaliza kidato cha nne mwaka wa 2019 alitoboa siri jinsi alimpata mwalimu akiiba sukari.

Kulingana na mwanamume huyo alikuwa katika shule ya wavulana ya miwaani.

"Siku moja nilimpata mwalimu akiiba sukari na kuekea mfukoni kwake, alipoona nimemuona aliniambia ya kwamba atanipa shillingi mia mbili ilininyamaze lakini alinikausha

Walimu walikuwa wanalalamika, hawajui mahali sukari inaenda kumbe ni mwalimu ambaye alifahamika kama Boniface alikuwa anaiba 

Nataka kumtobolea mwalimu mkuu na wanafunzi wa shule hiyo," Allieleza.