Nilijifanya kuwa mwendawazimu ili nisiendelee na masomo-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Nilijifanya kuwa mwendawazimu ili nisiendelee na masomo
Mbusi na Lion

Wakishindwa kuweka siri kwa kawaida huwa wanamwaya mtama kupitia kwenye kitengo cha toboa siri.

Je kuna mtoto wako amekusumbua kwa muda sasa hasa akiwa shule, lakini hujfahamu sababu kwanini anakusembua.

Mwanamume mmoja alisimulia na kutoboa siri jinsi alijifanya kuwa mwendawazimu kwa maana hakuwa anataka kuenda shule.

"Nikiwa kidatoo cha pili nilijifanya kwamba nimeshikwa na wazimu, sababu ya kujifanya sikuwa nataka kuenda shule wala kuendelea na masomo

Mama yangu alinipeleka hospitali lakini madaktari walikuwa wanasema kwamba niko sawa na sina tatizo lolote

Mimi ndiye kitinda mimba, kati ya watoto kumi na wawili,nilikuwa najifanya kuwa wazimu wangu ni wavita nakuchapa watu

Nilipelekwa kwa muhubiri na nikaombewa , misha nikapona, nilikuwa nikulizwa kwa nini nimekuwa wazimu nasema kwamba ni akinana mama watatu majirani walikuwa wameniroga kumbe ulikuwa ni uongo," Alisimulia mwanamume huyo.

Je amtobolee mama yake siri hii au akae nayo.