Mganga alinipa kifaranga mtu ambaye nimekuwa nikifanya tendo la ndoa naye-Mwanamume amwaya mtama

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri jamaa mmoja alwaacha mashabiki wa radiojambo na mshtuko baada ya kutoboa yale amekuwa akifanya baada ya kupewa kifaranga na mganga
  • Kulingana na mwanamume huyo usiku ukifika kifaranga huyo amekuwa akibadilika na kuwa mwanamke
Lion,DJ Nyce, na Mbusi
Image: Studio

Katika kitengo cha toboa siri jamaa mmoja alwaacha mashabiki wa radiojambo na mshtuko baada ya kutoboa yale amekuwa akifanya baada ya kupewa kifaranga na mganga.

Kulingana na mwanamume huyo usiku ukifika kifaranga huyo amekuwa akibadilika na kuwa mwanamke.

Lakini kwanini alienda kwa mganga na kupewa kifaranga huyo?

"Kuna msichana ambaye alikuwa ananikataa sana na nilikuwa nampenda sana, nilienda kwa mganga ili anitengenezee mambo ili anipende

Alinipa kifaranga kwa shilingi elfu nne, na kuniambia napaswa kumpa chakula na maji, na kunihakikishia mambo yangu yatkuwa sawa

La kushangaza ni kuwa usiku ukifika kifaranga huyo amekuwa akibadilika na kuwa mwanamke, nimekuwa nikifanya tendo la ndoa naye kwa muda wa wiki moja

Nataka kumtobolea mpenzi wangu kwamba nina jini mwanamke ambaye amekuwa nami, ndio maana sina hisia zake," Alieleza jamaa huyo.

Jamaa huyo alitaka kumtobolea mpenzi wake siri hiyo, na je ingekuwa ni wewe au ingekuwa ni mpenzi wako ungefanya nini baada yake kukutobolea siri kama hiyo.