Ndugu yangu aliniambia nifanye tendo la ndoa na mkewe ili wapate mtoto-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa aeleza jinsi alimpa mke wa ndugu yake ujauzito

Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama kwenye kitengo cha toboa siri, mwanamume mmoja alitooa siri jinsi walivyokubaliana na ndugu yake lakini mwishowe makubaliano yakageuka.

Kulingana na mwanamume huyo walikubaliana na ndugu yake afanye ngono na mkewe ili wapate mtoto kwa maana hana huwezo wa kumpa mkewe ujauzito.

PIa alisema makubaliano yao yalitoka baada ya ndugu yake kuwa na shinikizo kutoka kwa familia.

Usimulizi

"Ndugu yangu aliniambia nifanye ngono na mkewe ili apate ujauzito kwani hana uwezo wa kumpa mkewe ujauzito

Nilifanya vile tulikuwa tumekubaliana, sasa mkewe ana mtoto wa miezi saba, baada ya hayo ndugu yangu amekuwa akija nyumbani akiwa amelewa na kuana kunigombanisha

Alipoulizwa na wazazi alidai kwamba amenikopesha pesa na sijamregeshea ndio maana amekuwa akinigombanisha

Jana alimchapa mkewe, nataka kuwatobolea wazazi wangu kuwa sina pesa ya ndugu yangu lakini mtoto wake sio wake bali ni wangu na ni baada ya kukubaliana naye,"