Rafiki yangu alinituma nikapeleleze mpenzi wake,lakini nilimpachika mimba-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa atoboa siri, vile alimpachika mpenzi wa rafiki yake mimba
Mbusi,Lion na DJ Slim
Image: Studio

Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama kwenye kitengo cha toboa siri, ambapo wengi huwa wanatoboa siri ambazo wameshindwa kuziweka.

Siku ya Jumanne barobaro alitoboa siri jinsi alivyo mpachika mimba mpenzi wa rafiki yake.

Hii hapa siri yake;

"Kuna rafiki yangu ambaye alinituma nikampeleleze mpenzi wake, kama huwa anamcheza au anaweza kuwa na mpenzi mwingine

Nilimpa mpenzi wake maneno matamu, na kisha akakubali kuwa mpenzi wangu, pia nimempachika mimba na alikuja kanairo kunitembelea

Nataka kumtobolea rafiki yangu siri, kuwa alivyonituma nimemletea majibu, lakini mpenzi wake ana ujauzito wangu na ni mpenzi wangu sasa," Alitoboa.

Ni mambo ambayo yamekuwa yakishuhudiwa na ya kushangaza kila kuchao, huku wapenzi wakiuana kwa ajili ya udanganyifu.

Katika karne ya sasa wengi wanasema ni ngumu sana kumpata mpenzi akupendaye bila ya udanganyifu wowote je ni ukweli?

Jamaa huyo amtobolee rafiki yake siri au la?