Nilidangaya familia yangu naenda kujiua,wanadhani nimekufa-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa atoboa siri jinsi familia yake inadhani ameaga dunia
Lion,DJ Nyce na Mbusi
Image: Studio

Haya basi kuu wamekua wengi, na jamaa amemwaya mtama jinsi alitishia familia yake anaenda kujiua.

Umewahi ishi na familia lakini unahisi kwamba umetengwa na haupendwi kwa sababu ya kuonyeshwa madaharau na familia yako licha ya kutojua sababu yeyote.

Kuna dhana mbaya ambayo watu wengi wamekuwa nayo, kwamba mke wa pili au watoto wa mke wa pili hawapaswi kuwa na haki yeyote na ata ya kumiliki mali ya familia hiyo.

Je sababu ya kusema atajiua ni ipi?

"Familia yangu ilikuwa inanionyesha madharau na kuniambia kwamba mimi sio kijana wa hio boma, kwa sababu mama yangu alikuwa mke wa pili

Ilifika wakati nika choka na madharau yao, na nikatoka nyumbani na kuwaambia kwamba naennda kujiua, hamna mtu yeyote alinifuata kuni bembeleza

Baada ya kutoka nilienda kufanya kazi mjini, kuna wale wanaamini kwamba nimeaga dunia, na wengine wananitafuta

Nataka kuwatobolea siri ni waambie kwamba sijaaga dunia kwa maana sikujiua, na nimepata kazi nzuri na hivi karibuni nitarudi nyumbani," Alisimulia..

Hii hapa video mwanamume huyo akitoboa siri;