Watu wamekuwa wakitoroka wakiniona wakidhani mimi ni polisi wa DCI-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Jamaa atoboa siri jinsi watu wamekuwa wakimuita askari wa DCI
(Kushoto)Mbusi,(kati) DJ Nyce, (kulia) Mbusi
Image: studio

Haya basi kuku walikuwa wengi siku ya Jumatano, huku jamaa akimwaya mtama jinsi watu wamekuwa wakimuogopa.

Kulingana na jamaa huyo alitaka mawaidha ya wanajambo, kwani alidai watu wamekuwa wakimtoroka wakimuona huku wakidhani kwamba ni askari wa DCI.

Hii hapa siri yake;

"Watu katika mtaa wangu wamekuwa wakidhani kuwa mimi ni askari wa DCI, ni mwaka mmoja sasa watu waidhani kwamba ni askari

Mimi ni mlinzi wa usiku, cha kushangaza ni kuwa nikienda kununua kitu mahali kila mtu hutoroka wakisema kwamba mimi ni askari wa DCI

Yaani watu wamekuwa wakinitoroka, ata polisi wa kawaida,nataka kuwatobolea siri ni waambie kwamba mimi ni mtu wa kawaida na wala sio polisi

Nataka mashabiki wa radiojambo wanishauri nitafanya nini ili watu waache kuniogopa," Alieleza jamaa huyo.