Nimemwajiri mpango wangu wa kando kama kijakazi wangu-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Katika kitengo cha toboa siri, jamaa ameeleza jinsi amemwajiri mpango wake wa kando kama kijakazi wake

Wakishindwa kuziweka huwa wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri, je unamfahamu mke wako au mume wako vyema?

Karne hii ya sasa asilimia kubwa ya wanandoa hawatambui tamaduni za ndoa, kwani wamekuwa wakitafuta mipango ya kando ili kutimiza mahitaji yao.

Katika kitengo cha toboa siri, jamaa ameeleza jinsi amemwajiri mpango wake wa kando kama kijakazi wake.

Kulingana na mwanamume huyo, mkewe alimpa ruhusa ya kutafuta kijakazi kutoka kwao, na kumwendea mpango wake wa kando.

"Nimekuwa kwa ndoa kwa miaka 7, nimekuwa nikiajiri wafanyakazi na mke wangu anawafukuza kila mwaka

Aliniambia niende nikalete kijakazi kutoka kwetu nyumbani, nilienda na kumleta mpango wangu wa kando awe kijakazi wetu

Mke wangu hajui kama huyo ni mpango wangu wa kando, nataka kumtobolea siri nimwambie kwamba kijakazi huyo ni mpango wangu wa kando, kwa hivyo ajue ana mke mwenza

Nimetoboa siri hii, kwa sababu mpango wa kando alinitishia atamwambia mke wangu ukweli," Alisimulia

Je ni ushauri upi unawea mpa mwanamume huyu?