'Najua wewe ni mwizi,dada yako alinitishia nikuoe,'Mwanamke amtobolea mumewe siri

Muhtasari
  • Kipusa amtobolea mumewe siri jinsi alitishiwa ili amuoe

Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama kila siku ya juma, katika kitengo cha toboa siri.

Siku ya Jumatatu mwanamke alimtobolea mumewe siri, jinsi amegundua kuwa yeye ni mwizi.

Yote tisa kumi ni kuwa alimtobolea siri tena na kumwambia kwamba hampendi, na licha ya yote alitishiwa na dada ya mume wake amuoe.

Hii hapa siri yake;

"Nataka kumtobolea mume wangu wa miaka 2 kuwa nimejua kwamba yeye ni mwizi, kuna wakati tulienda nyumbani, kompyuta ya dada yangu ikapotea alipoulizwa alisema kwamba hajui ni nani amechukua

Kumbe alichukua na kumpelekea dada yake, pia nimekuwa nikinunua bidhaa za nyumbani kama nguo anachukua anaenda kuuza

Siri nyingine ni kuwa simpendi na nililazimishwa na dada yake ni muoe, alinitishia nisipomuoa ndugu yake nitapoteza kazi yangu."