Nimemnyakua mume wa rafiki yangu-Mwanamke atoboa siri

Muhtasari
  • Zikiwalemea wanatoboa, kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri kila siku ya juma
Mbusi,DJ Nyc na LIon
Image: Radiojambo

Zikiwalemea wanatoboa, kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri kila siku ya juma.

Katika kipindi cha toboa siri siku ya Jumatano mwanamke mmoja alimtobolea rafiki yake siri jinsi wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mume wake.

Kulingana na mwanamke huyo, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu humu nchini, na amekuwa akipewa maisha mema na mwanamume huyo.

Lakini siri iko wapi?Hii hapa siri yake.

"Nataka kumtobole rafiki yangu Mitchelle siri nimwambie kwamba nimemnyakua mume wake kwa muda sasa, na amekuwa akinipa pesa 

Mwanamume huyo alimwambia rafiki yangu ambaye ni mke wake kwamba ameenda mashambani lakini yuko kwangu, nataka kumtobolea rafiki yangu nimwambie kwamba mumewe hayuko mashambni bali yuko kwangu."

Kweli hawakukosea waliposema kikulacho ki kunguoni mwako.