Nimekuwa nikimtongoza shemeji yangu mitandaoni-Mwanadada amwaya mtama

Muhtasari
  • Mwanamke akiri kumtongoza shemejiye mitandaoni, ili kumjaribu kama ni mwaminifu kwa dada yake
Lion, MBusi, DJ Nyce
Image: Radiojambo

Ni mambo ambayo tumekuwa tukiyaona kwenye filamu na kushangazwa sana, na kushindwa kama yanaweza kufanyika kwenye maisha ya sasa.

Ndio yanaweza kufanyika na hata kuwaacha wengi midomo wazi, katika kipindi cha toboa siri mwanamke mmoja amewapa wengi butwaa baada ya kumwaya mtama yale amekuwa akimfanyia shemeji yake.

"Nilibadilisha nambari ya simu na sauti ili kumjaribu shemeji yangu nione kama ni mwaminifu kwa dada yangu

ananijua kama Rukia kwenye nambari hiyo nyingine, kwani tumeoanga kupatana lakini nataka kumtobolea siri  nimwambie kwamba ni mimi ambaye amekuwa akizungumza naye mitandaoni na kwenye simu yake,"Alieleza mwanadada huyo.

Yote tisa kumi ni kuwa alimfunga mumewe ili asiweze kutoa nje ya ndoa;

"MImi najua vyema mume wangu hawezi ni cheza kwani nilimfanyia mambo ili asinicheze, akinicheza tu kidogo atajua mimi ni mpokomo."

Huu hapa uhondo wote;

Mwanadada amtia majaribuni shemejiye kwa sababu ya kumshuku kwamba si mwaminifu kwa mkewe ambaye ni dadake. #ToboaSiri #MbusiiNaLionTekeTeke #OngeaUsikike

Posted by Radio Jambo on Wednesday, February 9, 2022