Nilivyonza elfu 100,000 za kuenda kanada-Jamaa atobolea kijiji chao siri

Muhtasari
  • Katika kipindi cha Mbusi na Lion teketeke, katika kitengo cha toboa siri, jamaa alitoboa siri jinsi alivyonza pesa za kuenda kanada kusoma
Image: Radiojambo

Katika kipindi cha Mbusi na Lion teketeke, katika kitengo cha toboa siri, jamaa alitoboa siri jinsi alivyonza pesa za kuenda kanada kusoma.

Kulingana na jamaa huyo alifanyiwa harambee na wazazi wake paoja na wanakijiji ili aweze kuenda lakini baadaye alikula pesa zote mwaka jana.

Pia alifichua siku ambayo alipokea pesa hizo alitumia zaidi ya elfu thelathini akijifurahisha na marafiki zake kisha wakamtoka.

Hii hapa siri yake;

"Ntaka kuwatobolea wazazi wangu na wanakijiji ambao walinichangia pesa ili niende Kanda kusoma, kwamba nilivyonza pesa zote mwaka jana na kuwa nimekuwa nikiwadanganya kwamba mambo hayajakuwa laini ili niweze kusafiri

Nilivyonza na marafiki zangu pesa kisha wakanitoroka, pia nilizungumza na Miguna ambapo tulikuwa tumeamua kukutana baada yangu kuwasili kanada

Nilikuwa nimepata udhamini wa masomo kutoa kwa mjomba wangu ambaye amekuwa akinisaidia."