Baba mkwe alinipachika mimba-Mwanadada amtobolea mumewe siri

Muhtasari
  • Alikiri kwamba baada ya kumuoa na kumuacha nyumbani, baba yake alichukua husukani na hata kumkodishia nyumba sokoni

Katika kitengo cha toboa siri katika Rdaiojambo, mwanadada alimwaya mtama baada ya kuku kuwa wengi.

Kulingana na mwanadada huyo licha ya kuolewa na mumewe, amepachikwa mimba na baba mkwe.

Alikiri kwamba baada ya kumuoa na kumuacha nyumbani, baba yake alichukua husukani na hata kumkodishia nyumba sokoni.

Hii hapa siri yake;

"Nataka kumtobolea mume wangu siri nimwambie kwamba ujauzito nilio nao wa miezi saba sio wake bali ni wa baba yake mzazi, ulinioa na kuniacha nyumbani kwenu

Ukweli ni kuwa kwamba ujauzito ni wa baba yako, na kwamba siyuko kwetu baba yako amenikodishia nyumba sokoni ili awe akinitembelea vyema." Alitoboa siri mwanadada huyo.

Je hiyo ni laana au ni mapenzi yalizidi baada ya mumewe kuondoka?