Rafiki yangu amekuwa akidhani mkewe ni dada yangu-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • NI nadra sana kupata ndoa ya wakati huu wa sasa zikidumu sana kwani, wengi wao hawana heshima kwa wenzi wao na kila mmoja anajiona kwama anajua zaidi ya yule mwingine
Mbusi na Lion

Ndoa za karne hii ya sasa na wakati huu wa sasa zina siri nyingi kuliko ndoa za akina babu zetu.

NI nadra sana kupata ndoa ya wakati huu wa sasa zikidumu sana kwani, wengi wao hawana heshima kwa wenzi wao na kila mmoja anajiona kwama anajua zaidi ya yule mwingine.

Kuku wakiwa wengi au wakishindwa kuweka siri na kisha kuwachoma roho huwa wanafungua roho kwenye kitengo cha toboa siri na kumwaya mtama.

Siku ya Jumatano jamaa mmoja aliwaacha mashabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri jinsi amekuwa akimpiga mke wa rafiki yake kuni.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nataka kumtobolea rafiki yangu siri kuwa mke wake sio dada yangu kama vile amekuwa akifikiria, mke wake ni rafiki yangu wa karibu ambaye nimekuwa nikifanya tendo la ndoa naye yaani nampiga kuni

NIkienda kuwatembelea rafiki yangu amekuwa akiniita shemeji na hata kuninunulia nyama na kuku ili nipikiwe na mke wake, kutoka leo nataka ajue kwamba huyo mke wake sio dada yangu kama tulivyomwambia awalai."