Niliiba simu ya aliyekuwa mpenzi wangu kulipiza kisasi-Jamaa amwaya mtama

Muhtasari
  • Kulingana na jamaa huyo aligundua kwamba mpenzi wake alikuwa anamcheza ilhali alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi naye
Mbusi na Lion

Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kipindi cha toboa siri ambacho wengi wamemwaya siri zao ambazo wameshindwa kuziweka na wamechomwa nazo.

Jamaa mmoja aliwaacha shabiki wa Radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri jinsi alijilipizia kisasi baada ya kuachana na mpenzi wake.

Kulingana na jamaa huyo aligundua kwamba mpenzi wake alikuwa anamcheza ilhali alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi naye.

Jamaa huyo alifichua kwamba baada ya kugundua kuwa mpenziwe ana wanaume wengi, alimtafutia mwanamume ili amtumie kisha kumuacha.

Hii hapa siri yake akimtobolea aliyekuwa mpenzi wake;

"Nilikuwa na mpenzi ambaye alikuwa anawapenda wanaume sana, niligundua kwamba sio mimi pekeyangu ambaye niko kwenye maisha yake baada ya kuachana nilimtafutia mwanamume ambaye alisoma katoba naye alipokuwa anasoma katiba niliingia kwenye nyumba yake na kuiba simu ya mpenzi wangu ili nilipize kisasi

Nataka kumtobolea siri ni mwambie kwamba simu yake haikupotea bali ni mimi niliiba, na kuwa mwanamume huyo ambaye yuko naye hampendi ni mimi jilimuunganisha naye bla kujua."