Jamaa mmoja siku ya JUmanne wakati wa kipindi cha toboa siri aliwaacha mashabiki nwa Radiojambo na mshangao baada ya kutoboa siri jinsi alivyo mfunga aliyekuwa mpenzi wake.
Kulingana na jamaa huyo, alimfunga ili asiweze kumpata mpenzi au kupata ujauzito.Alitoboa haya huku akisema alifanya haya kwa sababu kipusa huyo alimkosea sana.
Zaidi ya yote jamaa huyo ni msanii wa Hip Hop, ambaye alimtobolea kipusa huyo siri na kumwambia ya kwamba anataka kumfungua.
Hii hapa siri yake;
"Nilimfunga aliyekuwa mpenzi wangu ili asiweze kumpata mpenzi maishani mwake. nilifanya haya baada yake kunikosea sana, hata hawezi pata ujauzito kutokana na jinsi nilivyomfunga na uganga kupitia nguo zake za ndani
Pia amenidhibitishia haya kwani amekuwa akifanya ngono na wanaume lakini wanashikana kwa masaa 4,mimi ni msanii wa hip hop, lakini nataka nimfungue kwani najua ameteseka sana
Mimi nina wapenzi zaidi ya wawili."
Kweli yalimwengu hayatawahi isha, wala hatutawahi acha kuyashuhudia kwani kila siku siri baada ya siri zinatobolewa na kuwaacha wengi wameduwaa na kushindwa kama wanaishi katika dunia moja na wanaotoboa siri hizo.