Jerusalema: Kutana na Nomcebo Zikode ambaye sauti yake imeupamba wimbo maarufu wa Jerusalema
- Nilikuwa nimepoteza matumaini ,Jerusalema imejibu maombi yangu
- Wimbo wenyewe umechezwa mara milioni 55 katika Spotify
- Master KG ameijipatia mashabiki milioni 9 kila mwezi katiKa Tiktok ambapo wimbo huo umetazamwa mara milioni 385!
Msanii ambaye sauti yake ndio inayosikiza katika wimbo maarufu kwa sasa Jerusalema Nomcebo Zikode anasema alishangazwa jinsi wimbo huo ulivoteka ulimwengu mzima kwani wakati akiuimba studuioni akiwa na na DJ wa Afrika kusini Master KG hakujua kwamba kazi hiyo ingekuwa ya kutambulika kote .
Iwapo hadi sasa hujui Jerusalema ni wimbo upi au hata hujaona shindano la kudensi wimbo huo ambalo kila mtu ,kampuni ,mashirika ,vikosi vya usalama na wafanyikazi mbali mbali wameshiriki ,basi upo katika ulimwengu wako.Wimbo wenyewe ulikuwa tayari umetaka masafa ya Afrika kusini mwezi disemba mwaka jana , na katika mwaka mpya wa 2020 kufikia Oktoba sasa ndio umesambaa ulimwengu mzima . Zikode alikorekodi kibao hicho usiku mmoja karibu na mji wa Johannesburg na anasema alikuwa akipitia mengi na hata alikuwa ashaanza kupoteza matumaini . Akiwa kwake , Master KG alimpigia simu aj akasikize biti nzui ambayo alikuwa ametayarisha na alimtaka atafute mistari ya wimbo ambao wangeweza kuutengeza kwa biti hizo .
The video could not be loaded.
Alipojuja na kusikiza biti hizo alipendezwa mazo lakini akamtaka Master G amruhusu aende nazo nyumbani asikize Zaidi .Master G alikataa kumpa akimtka asilikilize pale studioni .Muda mfupi baadaye , Zikode alipata mistari ya kufoka na wakarekodi wimbo huo hadi saa sita usiku .wakati huo hawakujua kwamba kibao hicho kufikia mwaka huu kitakuwa na umaarufu kote na kimetazamwa katika Youtube mara zaidi ya milioni 170 .
‘ Yote haya yalifanyika wakati nilikaribia kupoteza matumaini’ anasema . Zikode amekuwa muimbaji wa pembeni kwa muda mrefu na alitaka tu sauti yake kusikika na wimbo wenyewe ulikua kama duala kwa Mola kutimiza ndoto yake .
Tangu wimbo wenyewe kutolewa Afrika kusini mwishoni mwa jana ,umekuwa ukichezwa kote na katika chati za kimataifa umejipata katika tano bora kwenye nchi za Belgium, France, Hungary, Netherlands Switzerland
Wimbo wenyewe umechezwa mara milioni 55 katika Spotify, ambapo MasterKG ameijipatia mashabiki milioni 9 kila mwezi katiKa Tiktok wimbo huo umetazamwa mara milioni 385!
The video could not be loaded.