Aliyekuwa mchekeshaji wa Churchill show Chipukeezy amewaacha mashabiki wake na hofu baada ya kufichua kuwa amelazwa hospitalini.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Chipukeezy aliposti picha na kuandika ujumbe mfupi unaosoma kama vile ufuatao;
"Mwanamume chini, afueni ya haraka Kasee." Chipukeezy Aliandika.
Hata hivyo hakufichua alichokuwa anaugua na amekuwa katika hospitali kwa muda gani, Chipukeezy amekuwa akiwasaidia wachekeshaji chipukizi humu nchini.
Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.