'Mtu amwambie Mejja si lazima ashirikishwe kwa kila wimbo,'Shakilla amshambulia msanii Mejja
- Mwanasosholaiti Shakilla amshambulia msanii Mejja hii ni baada ya kushirikishwa kwa kibao chake Bensoul cha 'Nairobi'
Mwanasosholaiti chipukizi Shakilla kwa mara nyingine ameanzisha ugomvi kati yake na msanii Mejja Khadija.
Hii ni baada ya msanii huyo kushiikishwa katika kibao cha Bensoul cha 'Nairobi'.
Kwa kweli tunamfahamu Shakilla kwa mambo ambayo amefanya kwenye mitandao ya kijamii na kuacha wanamitandao midomo wazi.
Awaki mwansosholaiti huyo alikuwa kwenye kipindi cha mchekeshaji Eric Omondi cha 'Wife material' ambapo baada ya Eric kumchagua mkewe Shakilla alidai kwamba ana ujauzito wake Eric.
Kwa wasanii wote ambao wamejaa humu nchini Shakilla alimua kumshambulia Mejja.
Ni kibao ambacho kilitoka siku ya Ijumaa,15 Januari ambapo kimewashirikisha wasanii tofauti lakini Shakilaa akaamua tu kumshambulia Mejja.
Kupitia kwenye mitandaoo yake ya kijamii ya instagram alikuwa na haya ya kusema kuhusu msanii huyo;
"Mtu amwambie Mejja si lazima kwake kushirikishwa katika kila wimbo,kibao cha Nairobi kilikuwa kizuri hadi pale alianza kuimba mistari yake
Anakaa Amin Dada mwenye gharama ya chinisekunde zake tatu hazikuhitajika, wacha mistari yake ifutwe na kibao hicho kiwekwe tena kwenye youtube kabla muda hauja yoyoma."Aliandika Shakilla.
The video could not be loaded.